Jinsi mtoto anavyokua.
Katika umri huu,mtoto wako atakuwa anapiga kelele pale anapokua amekasirika, japokuwa inaweza kukasirisha kumbuka anafanya vile si kwa sababu ni mkaidi ila ni njia yake pekee ya kuonyesha kuwa amekasirishwa na hawezi kufikiria vizuri kwa muda huo.
Mkumbushe mtoto kuzungumza mara kwa mara ikiwa ndo njia pekee ya kumsaidia kuongea haraka, mpongeze anapoonyesha utayari wa kujaribu kuongea, kwa muda muafaka jitahidi kuwa na mawasiliano mazuri na mwanao
Vilevile mfahamishe mtoto kuwa si salama kukimbia kimbia mtaani pasipo kushikilia mikono wako, zungumza naye kwanini si salama, ili aaweze kuelewa sababu za kumuonya.