Mtoto Miaka 2 na Miezi 3 – (Miezi 27)

Jinsi mtoto anavyokua

Katika siku hizi mtoto wako anajimudu kupiga hatua. Pia anaweza kubeba vitu vidogo na kucheza navyo kwa urahisi.

Mtoto wako sasa anaweza kutumia muda kutulia sehemu moja katika hali ya kuzubaa anapotatua baadhi ya mambo,hapenda kukatishwa .

Mtengenezee mikakati mizuri iliyo bora kama vile “utacheza na tofali kwa dakika 5 kisha ni wakati wa kula chakula cha jioni” ni vema kumpa onyo kabla ya kumshinikiza amalize michezo yake.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.