Jinsi mtoto anavyokua
Kwa sasa, kuna uwezekano mtoto wako akajua kutumia maneno 50 na kutengeneza sentensi kwa maneno rahisi mawili, kwa kufuata hatua za kuamuru kama vile “tafadhali chukua viatu vyako na umpatie baba”.
Kuna wakati unaweza kumuelewa anachosema lakini si mara zote utamuelewa hadi atakapotimiza miaka 4. Wakati mwingine watoto wadogo wanachanganyikiwa kuelewa mke na mume hivyo utatakiwa kumsaidia mtoto kuelewa.
Mtoto wako ataendelea kuwa mwembamba hata katika mwaka wake wa pili wa kuzaliwa kwa sababu kwa wakati huu kichwa chake kinakua taratibu sana na mikono na miguu vinaongezeka urefu na kuufanya mwili wake kuwa kama wa mtu mzima.
Utagundua kwamba, mtoto wako hali vizuri lakini endelea kumpatia vyakula vyenye virutubisho. Mlo wake unawezekana kuwa kamili zaidi ya unavofikiri. Kama unadhani mtoto wako hakui kama inavyopaswa, mpigie daktari wako anaweza kukutoa wasiwasi.