Jinsi mtoto anavyokua
Heri ya siku ya kuzaliwa! Inaweza kuonekana kama jana tu mtoto wako amezaliwa lakini mtoto wako ana miaka miwili. Mwaka jana mwanao alianza kukimbia, kutembea na kuchunguza vitu vilivyo mkononi mwake.
Mwaka huu uwezo wa mwanao kufikiri utakua. Ataanza kuwaza na kutengeneza picha ndani ya akili yake na kupangilia vitu vizuri. Kumbukumbu yake inaimarika. Akili ya mtoto wa miaka miwili itaweza kujua majina ya rangi muhimu. Wengine wanaweza kuhesabu mpaka tano.
Unaweza kuongea sentensi mbili mpaka tatu na mwanao sasa. Anajifunza maneno mapya kwa kutumia misamiati sahihi, na ataanza kujielezea vizuri pale anapohitaji kitu. Anapozidi kukua ataweza kujielezea yeye mwenyewe kama nini anapenda na nini hapendi. Maoni haya yanaweza kuleta mafarakano. Jaribu kuelewa hisia za mwanao na mhimize ashirikiane na wewe.