Baadhi ya mikao ambayo unaweza kujaribu ni pamoja na:
- Kusimama
- Kutembea tembea kadiri uwezavyo
- Kukaa
- Kuchuchumaa na kuegemea kiti, kitanda au mwenza wako
- Kupiga magoti na kuegemea mahali
- Kutambaa (Inaweza ikapunguza maumivu makali ya mgongo)
Kama mikao yote hii inakuletea shida na haisaidii na unaona kujilaza kwa mgongo ndio husaidia, jaribu kulala upande upande ukiwa umeweka mto kukusaidia. Vile vile kama ulivyokuwa unalala katika miezi 6 iliyopita.