Wakati huu mtoto anakua huru na makini sana katika mazingira nayomzunguka kwahivyo kuboresha mazungumzo kati yenu kuna msaidia kuendelea katika kutambua maneno. Pia wakati huu pua zake zitaendelea kuboreka. Kipindi hichi mtoto anajifunza yafuatayo ikiwa utajihusisha naye sana katika mazungumzo kwa kutumia vitu vifuatavyo:
Mazungumzo kwa bomba
Ni rahisi na nzuri.
- Unaweza kutengeneza mfano wa bomba karatasi au plastic
- Sehemu ya kwanza ya bomba weka kwenye sikio lake na sehemu ya mwisho jaribu kuzungumza taratibu
- Jaribu kumuambia maneno kama “habari mtoto”
- Anza kuongea kwa kumuigiza mtoto ili aweze kuzoea sauti yako
Midoli ya kuchezea
Utahitajika kumtafutia mtoto midoli, unaweza kutengeneza nyumbani au kununua sokoni
- Ichukue taratibu na kuipeleka eneo alilopo mtoto
- Subiri hadi avutiwe kuitazama
- Itambulishe midoli kwa majina rahisi kama vile “habari naitwa panya Jerry”
- Ifanye midoli kuzungumza katika hali ya utani , itamfanya mtoto kufurahia mazungumzo