Sasa mtoto wako anajaribu kusimama, ataimarika mikono yake na macho kipindi hiki. Unaweza kumsaidia kwa kumpatia vishughuli vichache ili kuboresha uwezo wake.
Michezo ya kurusha miguu
Zoezi hili litamsaidia vema mtoto katika uimarikaji wake
- Mshikilie mtoto kwa upande wa nyuma , mkono mmoja ukimshika kifuani mwake na wa pili ukimsaidia kwa chini.
- Weka mpira mbele ya miguu yake
- Sasa msaidie kupiga mpira huku ukiwa umemshikilia.
- Sema “piga” kila wakati na atafanya hivo.
Kelele
Mwanao atapenda kupiga kelele. Hivyo mpe vitu vya kumsaidia kufanya hivo
- Unaweza kumpatia sahani na kijiko ikiwa umemuweka katika kiti chake cha kukalia na kumfanyia sauti anayoitaka.
- Mwanao sasa atataka kutengeneza sauti kama hiyo kwa mikono yake mwenyewe.