Wakati huu mtoto anaendelea katika hatua nyingine ya mawasiliano. Unaweza kucheza naye michezo ya kuingiliana na akashiriki kwa haraka
Kurusha miguu
Mpendwa wako ataupenda mchezo huu
- Weka kiasi maji inchi 3 hadi 4 kwenye beseni la mtoto.
- Mkalishe wima kwenye maji kumruhusu aweze kurusha rusha miguu yake kwenye maji
- Kadri anavyorusha miguu ndivyo jinsi maji yanazidi kumwagika , hii itamfanya kufurahia sana mchezo huu.
Kutambaa
Mchezo huu utasaidia kumpa mtoto ujuzi wa kutosha
- Katika mwezi wa nne mtoto anapendelea kuanza kusogea.
- Wakati anajaribu kujivuta muwekee kitu chochote mbele yake mbali kidogo na mikono yake.
Mtazame mtoto anavyojaribu kujivuta mbele kadiri unavyosogea