Wakati huu mtoto ana miezi miwili na uwezo wake wa kuhisi unaongezeka mshirikishe sauti na vitu vya kuhisi. Anaweza kuhisi vitu vifuatavyo:
Vitu vinavyotoa sauti: utamuona mtoto anaanza kuitikia kelele, sauti tofauti za mziki, ngoma na sauti zinazotoka jikoni nk.
- Anza kutengeneza sauti mbalimbali, mtoto ataanza kuzizoea.
- Unaweza kutengeneza karatasi au midoli inayotoa kelele na mwanao ataanza kuifuatia kwa haraka.
Michezo ya kuruka: katika mwezi wa pili mtoto atafurahia michezo ya kusogea huku akizidi kuimarika.
- Fanya hivi kwa tahadhari, kwanza kaa chini
- Lala chini na uanze kupishanisha miguu juu chini
- Sema “juu, chini” kama ambavyo mtoto anatazama
- Furahia haya