Kipindi hiki kichanga anaanza kutambua vitu vinavyomzunguka, anatazama na kujaribu kuelewa mazingira yanayomzunguka. Wakati huu uwezo wa mtoto wa kuona una kikomo. Anaweza kuona vitu kuanzia inchi 8 hadi 10 kutoka umbali aliopo, kipindi hichi pia uwezo wake unaboreka katika kuhisi, kuona na kutambua sauti. Unaweza kumuandalia vitu kwa ajili ya kuchezea
Vichekecha: watoto wanapenda sana kuchezea vichekecha, sauti zake pia zinamsaidia mtoto katika mfumo wa kuhisi. Unaweza kuanza kwa kuchukua kichekecha kidogo na kufanya yafuatayo kwa ajili ya mtoto:
- Jaribu kuweka kichekecho katikati ya vidole vya mtoto
- Ingawa bado ni mdogo kushika ila atahisi uwepo wa kitu.
- Unaweza pia kutikisa kichekecho taratibu upande mmoja kwenda mwingine, itamsababishia kupepesa macho kufuatia mlio wa kichekecho.
- Jaribu usitikise kwa sauti kubwa itamfanya mtoto kuogopa.
Maongezi ya furaha: unahitaji kuwa na mawasiliano ya karibu sana na kichanga
- Wakati huu anajitahidi kuelewa vitu na sauti zinazomzunguka.
- Atajaribu pia kuwasiliana na wengine kwa sauti za ishara.
- Atajaribu kuzungumza kwa furaha na mtoto mwingine.
- Jitahidi kufanya vitu vya kumchekesha na kumfurahisha kwa sauti na sura za kuchekesha vitamsaidia kuzid kutambua vitu