Matatizo ya Kiafya Yanayohusiana na Ujauzito

Baadhi ya matatizo ya ujauzito yanatokea hata kwa wanawake wenye afya. Baadhi ya vipimo vinavyofanywa kipindi cha ujauzito vinaweza kukusaidia kujikinga na matatizo haya au kuyagundua mapema. Wasiliana na daktari wako mapema na kupata ushauri kuhusu matibabu ya tatizo utakalogundua.  Kwa kufanya hivyo utaongeza nafasi ya kujifungua salama na mtoto mwenye nguvu na afya. Lifuatalo ni jedwali linaloonyesha badhi ya matatizo yanayohusiana na ujauzito, dalili na matibabu yake:

Matatizo ya kiafya wakati wa ujauzito
Tatizo Dalili Tiba
Anemia – upungufu wa damu(chembe nyekundu zenye afya za damu)
  • Kusikia kuchoka au mnyonge
  • Kupauka
  • Kuhisi kuzimia
  • Kupungukiwa pumzi
Kutibu chanzo cha “anemia” inaweza kusaidia kurudisha idadi ya chembe nyekundu za damu zenye afya. Wanawake wenye matatizo yanayohusiana na “anemia” wanasaidiwa kwa kutumia madini chuma na virutubisho vya foliki asidi. Daktari wako atachunguza kiwango cha chuma kipindi chote cha ujauzito wako kuhakikisha “anemia” haitokei tena.
Msongo wa mawazo– Huzuni wakati wa ujauzito au baada ya kuzaliwa (baada ya kujifungua)
  • Huzuni kubwa
  • Mabadiliko ya hamu ya kula
  • Mawazo ya kujiumiza wewe au mtoto.
  • Kujisikia kukosa msaada na mwenye hasira.
Wanawake wenye ujauzito wanaweza kusaidiwa kwa matibabu kama:

  • Ushauri nasaa
  • Makundi ya kusaidiana
  • Dawa

Msongo wa mawazo wa mama unaweza kuathiri ukuaji wa mtoto, hivyo kupata tiba ni muhimu kwa mama na mtoto.

Mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi,mara nyingi kwenye mirija ya falopiani.
  • Maumivu ya tumbo la uzazi
  • Maumivu ya mabega
  • Kutokwa damu ukeni
  • Kusikia kizunguzungu au kuzimia
Madawa au upasuaji hutumika  kutoa mtoto mchanga ili viungo vyako vya uzazi visiharibike.
Matatizo ya mtoto tumboni – mtoto aliye tumboni ana matatizo ya kiafya,kama ukuaji hafifu au matatizo ya moyo.
  • Mtoto kusogea kuliko kawaida
  • Mtoto kuwa mdogo kuliko kawaida.
  • Matatizo mengine hayana dalili, ila yanagundulika kwa vipimo vya hospitali.
Matibabu yanategemea majibu ya vipimo vinavyochunguza afya ya mtoto. Kama kipimo kimegundua kuna tatizo, haimaanishi mtoto yupo katika hatari sikuzote. Inaweza kumaanisha mama anahitaji kuangaliwa kwa makini mpaka mtoto atakapozaliwa.Hii inajumuisha vitu vingi kama mama kupumzika kitandani. Wakati mwingine mtoto anatakiwa kuzaliwa mapema.
Ugonjwa wa kisukari kipindi cha ujauzito– kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu wakati wa ujauzito
  • Kawaida hakuna dalili. Wakati mwingine kiu kali, njaa au uchovu
  • Uchunguzi wa vipimo kuonyesha viwango vikubwa vya sukari kwenye damu.
Wanawake wengi wajawazito wenye matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari wanaweza kudhibiti kwa kufuata utaratibu wa mlo wenye afya kutoka kwa daktari. Wanawake wengine wanahitaji “insulin” kuweka viwango vya sukari kwenye damu chini ya udhibiti.  Kufanya hivyo ni muhimu kwa sababu ugonjwa wa kisukari ukipuuziwa unaongeza hatari ya:

  • Kifafa cha mimba
  • Kujifungua kabla ya mda
  • Kujifungua mtoto mkubwa, inaweza sababisha ugumu wakati wa kujifungua
  • Upasuaji wakati wa kujifungua.
  • Mtoto kuzaliwa na kiwango kidogo cha sukari ndani ya damu,matatizo ya kupumua, na manjano
Shinikizo kubwa la damu– shinikizo kubwa la damu linaanza baada ya wiki ya 20 ya ujauzito na kupotea baada ya kujifungua
  • Shinikizo kubwa la damu bila ishara au dalili za kifafa cha mimba.
Afya ya mama na mtoto kuangaliwa kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha shinikizo kubwa la damu sio kifafa cha mimba.

.

Hyperemesis gravidarum (HG) – ugonjwa huu unahusisha kutapika na kusikia kichefuchefu kuliko kawaida wakati wa ujauzito-ni zaidi ya magonjwa ya asubuhi ya mama mjamzito ambayo ni kawaida.
  • Kichefuchefu kisicho na mwisho
  • Kutapika mara nyingi kila siku
  • Kupoteza uzito
  • Hamu ya kula kupungua.
  • Kuzimia au kusikia kuzimia
  • Kukosa maji mwilini
Vyakula vikavu, na vyakula maalumu ambavyo ni laini,vilivyopikwa na visivyo na pilipili na vinywaji  ni hatua ya kwanza ya tiba ya hali hii. Wakati mwingine dawa zitakusaidia kupunguza au kuondoa kichefuchefu. Wanawake wengi wenye tatizo hili hulazwa hospitalini ili wapewe vimiminika na virutubisho vya kutosha.Kawaida wanawake wanaosumbuliwa na tatizo hili hupata nafuu kuanzia wiki ya 20 ya ujauzito. Lakini baadhi ya wanawake wanatapika na kusikia kichefuchefu kipindi chote cha mimba.
Mimba kuharibika–Asilimia 20 ya mimba zinaishia kuharibika kabla ya wiki ya 20. Mara nyingi mimba iharibika kabla ya mwanamke kugundua ni mjamzito. Ishara za kuharibika mimba ni kama:

  • Kuona madoadoa ya damu ukeni.
  • Kuumwa tumbo na maumivu chini ya kitovu.
  • Kutokwa maji au tishu(mabaki ya kijusi) ukeni
Mara nyingi, mimba kuharibika haina kinga. Mwanamke anahitajika kufanyiwa matibabu ya kuondoa tishu zote za kijusi ndani ya mfuko wa mimba. Ushauri nasaha unaweza kusaidia kuponya hisia za kupoteza mtoto.
Placenta previa – ni tatizo la kitaalamu  linalohusisha plasenta kufunika shingo ya mfuko wa mimba,hivyo kuingilia uzalishaji wa mtoto kwa njia ya kawaida.
  • Kutokwa damu ukeni bila maumivu wakati wa miezi mitatu ya pili ya ujauzito au miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito.
  • Wakati mwingine hakuna dalili
Ikiwa itagundulika baada ya wiki ya 20 ya ujauzito, na hakuna damu inayotoka,mwanamke atahitajika kupunguza kazi zake na kuongeza mapumziko kitandani. Ikiwa damu inatoka kwa kasi,mama mjamzito atahitajika kulazwa mpaka mama na mtoto watakapokua salama. Ikiwa damu imeacha kutoka au kupungua mama anatakiwa kuendelea kupumzika kitandani mpaka siku ya kujifungua.

Na ikiwa damu inaendelea kutoka, au uchungu wa kujifungua umeanza kabla ya mda wake,mtoto atazaliwa kwa njia ya upasuaji.

Placental abruption Plasenta kutengana na ukuta wa mfuko wa uzazi kabla ya kujifungua, na mtoto tumboni kukosa oksijeni.
  • Kutokwa damu ukeni
  • Kuumwa tumbo la uzazi,kubanwa nyonga na kulainika kwa mfuko wa mimba.
Kama kutenganishwa kwa plasenta na ukuta wa mimba ni mdogo,mapumziko kitandani kwa siku chache yatasaidia kupunguza damu kutoka. Kwa hali ya katikati itahitaji mapumziko ya kudumu kitandani, lakini hali mbaya ya kutengana plasenta na ukuta wa mfuko wa mimba itahitaji matibabu haraka na mtoto kuzaliwa mapema.
Kifafa cha mimba– hali hii huanza wiki ya 20 ya ujauzito na kusababisha shinikizo kubwa la damu na matatizo kwenye kibofu na ogani nyingine.
  • Shinikizo la damu
  • Mikono na uso kuvimba
  • Protini nyingi kwenye mkojo
  • Maumivu ya tumbo
  • Kizunguzungu
  • Maumivu ya kichwa
Tiba kubwa ni kujifungua, ambayo inaweza isiwe salama kwa mtoto. Ikiwa kujifungua mtoto itakua mapema sana, daktari atamuangalia mama na mtoto kwa ukaribu sana, hivyo kulazwa hospitalini ni jambo la muhimu wakati huu. Matumizi ya dawa ni muhimu ili mama asipate mshtuko wa moyo.
Uchungu kabla ya muda wa kujifungua– kupata uchungu kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito.
  • Kuongezeka kasi ya kutoka majimaji ukeni
  • Shinikizo na kubanwa  kwenye nyonga
  • Maumivu ya mgongo
  • Kubana na kuachia tumbo la uzazi.
Dawa zinaweza kupunguza uchungu kuendelea. Inashauriwa kumpumzika kitandani. Wakati mwingine mama mjamzito anahitajika kujifungua mapema kabla ya wiki ya 37.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.