Mahitaji Muhimu ya Mtoto
- Diapers (Nepi)
- Wipes (taulo zenye maji): kwaajili ya kumfuta mtoto akijisaidia haja kubwa na haja ndogo.
- Sabuni nzuri kwaajili ya kufulia nguo za mtoto: watoto wanazaliwa na ngozi nyeti, ni vyema kuchagua sabuni nzuri na yenye harufu nzuri katika ufuaji wa nguo za mwanao.
- Mto wa kumbebea mtoto: mto huu utasaidia kuleta ahueni kwa mama hasa mgongoni, uti wa mgongo na mikono. Pia kwa wamama waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua unasaidia kupunguza mgandamizo kwenye kidonda. Dhumuni la kwanza la mto ni kumleta mtoto karibu na wewe na karibu na maziwa hasa wakati wa kumnyonyesha. Ni muhimu kuwa na mto ili kumsaidia mtoto kunyonya vizuri bila usumbufu.
- Vitambaa vya kumfuta mtoto: watoto wanacheuwa kila wakati, ni vizuri kuandaa vitambaa maalumu kwaaji;o ya kumfuta kila saa anapocheuwa au kutema mate.
- Bebeo la mtoto: sio kila mda utambeba mwanao akikuhitaji. Kuna mda utahitaji kutumia mikono yako, hivyo ni vizuri kutafuta bebeo la kumbebea.
- Chupa za mtoto: kama bado hujanunua chupa kwaajili ya kulishia mtoto maziwa na maji miezi sita ikifika, ni wakati mzuri wa kununua sasa.
- Pampu ya titi: kama utawahi kurudi kazini na mtoto hajafika wakati wa kuanza kula vyakula vingine, pampu ya titi itakusaidia kukamua maziwa kwaajili ya baadae ukienda kazini. Kumbuka maziwa hayo yaliokamuliwa ni vema yakahifadhiwa katika hali ya joto na kupewa mtoto katika hali ya uvuguvugu. Unaweza tumia maji ya moto kuhifadhi.
- Sabuni ya mtoto: ni vizuri kutumia sabuni maalumu za watoto kama family for baby au nyingineyo.ikiwa sabuni hizi zimemkataa mtoto jaribu kutumia sabuni ya kipande kama jamaa. Epuka sabuni zenye marashi makali kwa mtoto.