Kuna utofauti mkubwa kati ya kujua kulia ni kawaida, na kuwa na uwezo wa kukabiliana na vilio vya mara kwa mara kwa watoto.
Haijalishi ni kiasi gani unampenda mtoto au umejiandaa kuwa mzazi kama ulivyo. Upo katika hili tatizo, na kuwa katika tatizo inamaanisha lazima uchoke na kuzidiwa, na pia kujisikia kidogo usiye na msaada.
Haya yote ni kawaida. Usijilaumu pale unapoanza kusikia sauti ya mtoto wako kama misumari katika ubao. Haujafanya jambo lolote baya,na ni kawaida kukubali yote haya sio rahisi kuyadhibiti.
Pamoja na yote unayopitia, sio sawa kumuumiza au kumshtua mtoto wako ili aache kulia. Kwa hiyo cha kwanza na muhimu, kama unahisi unaweza ukapata hasira na kushindwa kujizuia, muweke mtoto kitandani salama na ondoka. Kuhitaji dakika chache mwenyewe hakukufanyi wewe kuwa mzazi mbaya. Na ili mradi umuweke mtoto katika sehemu salama asiyoweza kudondoka mtoto wako atakua salama.
Pia tafuta muda ambao ni wa kwako peke yako ukiweza. Hii ina maana kujipumzisha mtoto wako akilala, au kumuachia mwenza wako mtoto ili ukapate matembezi kidogo kwa lisaa au zaidi.
Wakati mwingine njia nzuri ya kukabiliana na hali hii ni kuhakikisha unajijali pia na wewe mwenyewe. Hakikisha unapata muda wa kupumzika kila siku hata kwa lisaa limoja, usije ukapata msongo wa mawazo.