Jinsi gani kipimo cha nyumbani cha ujauzito kinafanya kazi?
Mara baada ya mayai na manii kukutana, maumbile mbalimbali yanaunganika kutengeneza seli mpya. Seli hii mpya ingawanyika haraka, na kila seli mpya iliyoundwa kugawanyika tena na tena, kuwa kiini-tete.
Baadhi ya seli mpya ndani ya kiini tete hukua, na kufanyika plasenta ya mtoto. Hizi plasenta za mtoto huanza kutengeneza hCG kwa viwango vidogo hata kabla ya kiini-tete kujishikiza kwenye ukuta wa uterasi. Pindi kiini-tete kimejishikiza katika ukuta wa mji wa mimba, ndo kipindi inajulikana umeshika mimba, utengenezaji wa (hCG) unaongezeka na Hcg inaamrisha mwili kuachisha hedhi
Kiwango cha hCG katika mwili wako kinaongezeka kila siku mbili mpaka tatu kadiri kiini tete kinavyozidi kukua na plasenta yake inavyoendelea kuongezeka.
Wapi unaweza kupata kipimo cha mimba?
Unaweza kununua vipimo vya ujauzito, bila kuelekezwa na daktari, mtandaoni na katika maduka ya dawa na maduka makubwa. Unaweza pia kupata moja kwa moja kutoka kwa mshauri wako wa afya, kliniki ya uzazi wa jamii au kliniki ya afya ya uzazi.
Lini nifanye kipimo cha ujauzito?
Kufanya maamuzi ya lini kufanya kipimo cha ujauzito cha nyumbani imekuwa chanzo kikubwa cha wasiwasi kwa wanawake wengi hasa kama wanataka kushika mimba, lakini hata wakati mwingine wakiwa hawataki kushika ujauzito.
Iwe unataka kupata majibu chanya au hai ya kipimo cha ujauzito, kuchukua kipimo mapema inaonekana kama njia nzuri ya kupata majibu. Kwa bahati mbaya kufanya kipimo mapema inaweza kukupatia majibu hasi (-) hata kama una jujauzito.
Muda gani ni muafaka kufanya kipimo hichi?
Muda mzuri kabisa wa kufanya kipimo hichi ni baada tu ya hedhi yako kuchelewa (kama hedhi yako ilipaswa kuanza Jumatano, fanya kipimo Alhamisi kwa uhakika zaidi). Hii itakusaidia kuepuka majibu ya uongo. Ikiwa mzunguko wako wa hedhi haueleweki (irregular) usifanye kipimo mpaka utakapopita mzunguko mrefu unaokuwaga nao. Kwa mfano, kama mzunguko wako unacheza kati ya siku 30 mpaka 36, muda muafaka wa kufanya kipimo chako utakua siku ya 37 au zaidi ya hapo. Vinginevyo, subiri wiki tatu baada ya kufikiri unaweza kuwa na mimba kabla ya kufanya kipimo.
Hata hivyo, kila mimba ni tofauti, na kiwango cha hCG kinabadilika sana. Viwango vya hCG vinakua juu kileleni katika wiki karibia ya sita ya ujauzito. Hivyo, kipindi hedhi yako imechelewa wiki au wiki mbili, utaweza kupata majibu yenye uhakika.
Ikiwa umeacha kutumia dwa za uzazi wa mpango hivi karibuni, si rahisi kujua mzunguko wako wa kawaida. Ikiwa majibu yatakuja hasi(negative), jaribu tena kupima baada ya siku tatu.
Wakati gani wa siku ni mzuri kuchukua kipimo cha ujauzito?
Unaweza kupata majibu ya uhakika zaidi ikiwa utachukua kipimo chako asubuhi. Kipimo cha ujuazito cha nyumbani kinafanya kazi kwa kutambua homoni (Human chorionic gonadotropin-hCG) katika mkojo wako. Mkojo wako wa asubuhi utakuwa una viwango vikubwa isipokuwa kama uliamka katikati ya usiku kujisaidia aua ulikunywa maji uiku mzima. Hii inamaanisha kuwa wingi wa hCG utakuwa wa juu zaidi na kuna uwezekano mkubwa wa kupata majibu chanya kama una ujauzito.
Je, inachukua mda gani kupata majibu ya ujauzito?
Angalia maelekezo yanayokuja na kipimo, ila unaweza ona majibu baada ya dakika moja au mbili. Inaweza kuonekana kama ni mda mrefu kidogo!
Je, vipimo vya nyumbani ni vya uhakika?
Vipimo vya nyumbani vina uhakika kama ukifuata maelekezo yanayotolewa. Baadhi ya vipimo vina umakini wa kugundua haraka, rahisi kutumia na kutafsiri zaidi ya vingine. Umakini kugundua haraka katika kipimo ni mzuri zaidi maana unanyaka hata viwango vidogo vya hCG ndani ya mwili wako.
Ikiwa huwezi kusubiria mpaka utakapokosa hedhi yako, vipimo vya mimba vya kidigitali vinatajwa kuwa na uhakika zaidi.
Unaweza kujua umakini wa kipimo cha ujauzito cha nyumbani kwa kusoma habari inayokuja kwenye sanduku la kipimo. Utaona kuwa viwango vya hCG vinaripotiwa katika Units za Kimili (MIU) kwa mililita.
Udogo wa namba katika kipimo, ndio uharaka wa kipimo kugundua ujauzito zaidi. Kwa hiyo kipimo kinachoonyesha 10mIU / ml ni makini zaidi kugundua ujauzito katika mkojo zaidi ya kipimo cha k 40mIU / ml. Vipimo vyote vinasadikika kuwa na uwezo wa kutambua ujauzito asilimia 99 kwa uhakika ikiwa utachukua kipimo hedhi wakati muafaka.
Kuna utofauti gani kati ya vipimo vya nyumbani vya ujauzito na vile vinavyofanywa na daktari?
Madaktari wengi wanatumia vipimo vinavyotumika nyumbani kupima ujauzito kama wanataka kuhakikisha kama una ujauzito.
Daktari wako anaweza kupendekeza kufanya kipimo cha damu kama unaonyesha dalili za kuwa na ujauzito nje ya mirija ya uzazi au (molar pregnancy). Hizi zinahitaji matibabu mara moja.
Kipimo cha damu ni cha uhakika zaidi zaidi ya mkojo. Kinaweza kukujulisha kama una ujauzito mara tu baada tu ya urutubishwaji wa yai. Kipimo hiki ni kabla ya vipimo vya ultrasound havijaanza kutambua ujauzito.
IMEPITIWA: APRIL,2020.