Vifuatavyo ni vidokezo vinavyoelezea jinsi ya kumlisha mtoto kwa chupa katika hali ya usalama:
Hakikisha umekaa vizuri. Mkao utakao kusadia kumshika mtoto wako vizuri na kumuangalia machoni ukiwa unamlisha. Kumlisha mtoto kwa chupa ni nafasi nzuri ya kuwa karibu na mtoto wako na kumjua zaidi.
Mpakate mtoto wima ukiwa unamlisha kwa chupa. Shika kichwa chake vizuri ili aweze kupumua na kumeza vizuri. Anza kwa kuweka chuchu ya chupa kwenye midomo ya mtoto, mara atakapofungua mdomo mruhusu aivute chuchu ya chupa mwenyewe kwaajili ya kunyonya maziwa ndani ya chupa.
Daima mpatie mtoto mda wa kutosha wa kula.
Mtoto wako atahitaji mapumziko mafupi wakati unamlisha na atahitaji kucheua wakati mwingine. Ikiwa mtoto wako hataki kunywa maziwa tena, msimamishe wima, taratibu mpige ige mgongoni ili acheuwe.