Utungaji mimba hutokea kipindi yai la mwanamke linapokutana na seli za gamete za kiume zilizokomaa (manii). Inaweza chukua dakika 45 mpaka masaa 12 kwa manii kufika katika mirija ya falopiani ambapo mimba hutungiwa. Hata hivyo, manii yanaweza kuendelea kuishi ndani ya mwili wa mwanamke mpaka siku saba, hivyobasi utungaji wa mimba unaweza kutokea siku yoyote katika wiki ifuatayo baada ya kujamiana, kama upo katika siku za kutoa mayai(ovulation).
Ndani ya mwili wa mwanamke: jinsi yai linavyotungwa
Kwa wanawake, uwezekano wa mimba unaanzia katika ovari zake. Hizi ni ogani ndogo mbili zenye umbo la yai zilizoshikiliwa katika kila upande wa mjii wa mimba(uterasi). Ovari zimejazwa mayai ambayo yalitengenezwa kabla ya kuzaliwa. Kila mtoto mchanga wa kike anazaliwa na milioni 1 mpaka 2 ya mayai kwa kila ovari yake.
Mayai mengi yanaanza kufa mapema na mengine kupungua taratibu kadiri unavyozidi kukua. Mara unapoanza hedhi, kawaia kati ya miaka 10 na 14, ni mayai 600,000(laki sita) tu yanaweza kuwepo. Katika umri wa miaka 30, wanasayansi wamekokotoa ni ttakribani mayai 72,000 yanaweza kubakia.
Kuna uwezekano wa kuzalisha mayai 400-500 katika kipindi cha miaka yako ya kuzaa, ambayo ni kati ya hedhi yako ya kwanza na wakati wa kukatika hedhi.
Katika kila mzunguko wa hedhi,mara nyingine baada ya hedhi yako, kati ya mayai matatu na 30 yanaanza kukua katika kila moja ya ovari zako. Yai lililoiva linakua la kwanza kutolewa kupitia mfumo wa utoaji wa mayai(ovulation). Yai linamezwa na mirija ya falopiani iliyokaribu, kuna mirija miwili, kila mmoja una urefu wa 10sm, ambayo inaelekezwa kwenye mji wa mimba kutoka kwenye ovari.
Kawaida utolewaji wa mayai katika ovari(ovulation) ni takribani siku 14 kabla ya hedhi yako ijayo. Muda muafaka wa utolewaji wa mayai unategemea na urefu wa mzunguko wako wa hedhi. Homoni kadhaa wa kadhaa zinafanya kazi pamoja kudhibiti mzunguko wako, kukomaa kwa mayai na muda wa kutolewa mayai (ovulation).
Yai baada ya kutolewa huishi mpaka masaa 24 kwa wastani. Yai hili linahitaji kurutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mda huu ili mimba kutungwa. Kama yai likikutana na mbegu ya kiume yenye afya ikielekea kwenye mji wa mimba, utengenezaji wa kiumbe kipya unachukua nafasi. Kama sivyo, safari ya mwisho ya yai itakua kwenye uterasi na kuharibika.
Ikiwa haujashika mimba, ovari huacha kutengeneza homoni za estrogen na progesterone. Hizi ni homoni mbili ambazo zitasaidia kuhifadhi mimba. Wakati viwango vya homoni hizi vinashuka,ukuta mwembamba ndani ya uterasi unatolewa wakati wa hedhi yako.Mabaki ya mayai yasiorutubishwa hutolewa pia wakati mmoja.
Ndani ya mwili wa mwanaume: jinsi mbegu za kiume (shahawa) zinavyotengenezwa.
Miili ya wanawake hutengeneza yai moja kila mwezi. Hata hivyo miili ya wanaume, inakua katika kazi wakati wote, hutengeneza milioni za mbegu za kiume. Dhumuni pekee la kila mbegu ni kuogelea na kupenya kwa yai la mwanamke.
Kuanzia mwanzo mpaka mwisho inachukua karibu wiki 10 kutengeneza seli mpya ya mbegu ya kiume. Nusu ya mbegu zinazotengenezwa zinaishi wiki chache ndani ya mwili wa mwanaume, na angalau milioni 39 zinatolewa nje ya mwili (ejaculation).Ina maana kwamba wanaume wanapaswa kutengeneza mbegu mara kwa mara katika maisha yao yote ya utu wazima.
Homoni zinazodhibiti utengenezaji wa mayai(ovulation) kwa wanawake zinahamasisha utolewaji wa homoni ya testosteroni kwa wanaume. Testosteroni ni homoni inayohusika na kuzalisha manii. Uzalishaji wa manii huanza ndani korodani, tezi mbili zilizomo katika kifuko kilichokuwa chini ya uume.Korodani(mapumbu) zinapatikana nje ya mwili kwa sababu ni hatari kwenye mazingira ya joto. Ili kuzalisha mbegu bora yenye afya inapaswa kukaa kwenye digrii 34 za sentigredi. Hii ni karibia digrii nne pungufu ya joto la kawaida la mwili. Mara baada ya manii kutengenezwa, yanahifadhiwa katika kila korodani ndani ya mrija unaounganisha korodani na urethra, yenye urefu wa mita sita.
Kabla ya kumwaga mbegu nje ya mwili(ejaculation), mbegu hutolewa na kuchanganywa na shahawa.
Licha ya utengenezaji wa milioni za mbegu na utolewaji kwa njia ya kumwaga nje ya mwili(ejaculation), ni mbegu moja tu inaweza rutubisha kila yai. Jinsia ya mtoto wako inategemea na mbegu ya kwanza kupenya kwenye yai. Mbegu zenye kromosamu Y zinatengeneza mtoto wa kiume, na zile za X zitatengenza mtoto wa kike.
Nini hutokea wakati wa kujamiana
Pamoja na raha zote, miili yenu inatengeneza mvutano ambao utaishia kufika kileleni (climax). Kufika kileleni katika tendo la ndoa kuna kazi muhimu ya kibiolojia. Kwa wanaume, kufika kileleni husababisha shahawa kufika katika uke na kuelekea kwenye via vya uzazi kilomita 10 kwa saa. Kitendo cha kumwaga mbegu(ejaculation), hupatia mbegu mwongozo mzuri kuelekea kwenye yai la mwanamke. Mwanamke hana haja ya kufika kileleni ili mimba itungwe.mibano milaini ya kuta za uterasi zinaweza kusaidia mbegu ya mwanaume kusafiri vizuri kufikia lengo lake, lakini haya yote hutokea bila mwanake kufika kileleni.
Sio wanawake wote, miili yao inatoa yai katikati ya mizunguko yao au mda sawa katika mizunguko yao ya mwezi. Ili kuboresha nafasi yako ya kushika mimba, weka lengo la kujamiana kila siku mbili au tatu za mzunguko wako.
Wakati unapumzika baada ya ngono, kazi ya manii ndo kwanza inaanza
Katika kipindi hiki hakuna kubwa la kufanya zaidi ya kuomba jambo la kushika mimba lifanikiwe.wakati wewe na mwenzi wako mnafurahia tendo la ndoa, kuna mengi yanaendelea ndanu ya mwili wako. Mamilioni ya manii yameanza kazi yao ya kutafuta yai la mwanamke, na ijulikane kwamba hii sio kazi rahisi. Kipingamizi cha kwanza kinaweza kuwa uteute wa kizazi cha mwanamke ambayo unaweza kuonekana kama nyavu isiyoruhusu kuingia kwenye siku zisizofaa kurutubisha yai. Unapokuwa katika siku nzuri za kushika mimba, ni miujiza sana kwani uteute hu wa kizazi unapungua na kuruhusu mbegu yenye nguvu na kuogelea kwa kasi kuvuka.
Kwa mbegu ambayo imefanikiwa kuvuka bado ina safari ndefu mbele. Zinahitajika kusafiri karibia sentimita 18 kutoka kwenye uke kupitia kwenye uterasi(mji wa mimba) mpaka kwenye mirija ya falopiani. Ni mtihani mkubwa ukizingatia usafiri wake ni wa kiwango cha sentimita 2.5 kila dakika 15. Mbegu ya kiume yenye kusafiri kwa haraka zaidi inaweza kukutana na yai katika dakika 45. Inaweza kuchukua mpaka masaa 12 kwa mbegu ya kiume yenye kasi ndogo kufikia yai. Kama mbegu haijakutana na yai katika mirija ya falopiani mda wa kujamiana, inaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke mpaka siku saba. Hii ina maana yai likitolewa(ovulation) ndani ya huu mda unaweza kushika mimba.
Kiwango cha vifo vya manii ni cha juu sana na dazeni kadhaa tu huwahi kulifikia yai. Nyinine hukamatwa,kupotea(pengine kuelekea mrija wa falopiani ambayo sio) au kufa zikiwa katika safari. Kwa wachache wanaofanikiwa kulikaribia yai, bado mpambano ni mkali. Kila mmoja anahitaji kufanya kazi kwa kasi ili kupenya sheli ya nje ya yai na kupita ndani kabla ya wengine. Yai linatakiwa kurutubishwa ndani ya masaa 24 baada ya kutolewa. Mara baada ya manii yenye kazi na nguvu kufanikiwa kupenya kwenye yai, mara moja yai linabadilika na kuzuia manii nyingine kuingia kitendo hiki ni kama kinga inayotolewa na yai mara tu mbegu ya kwanza iko salama ndani.
Sasa maisha mapya yamezaliwa
Wakati wa urutubishaji(muunganiko wa manii na yai),maumbile katika manii na yai huchanganya kuunda kiini kipya ambacho kitaanza kugawanyika haraka. Mjumuiko huu wa seli mpya unajulikana kama blastocyst. Inaendelea kusafiri kutoka kwenye mirija ya falopiani kwenda kwenye mji wa mimba, safari inayochukua siku tatu au zaidi.
Huwezi kuwa mjamzito mpaka mjumuiko wa seli(blastocyst) ijishike yenyewe kwenye ukuta wa uterasi ambayo itakua kijusi na plasenta. Mara nyingine, blastocyst ijishikisha mahali pengine mbali na mji wa mimba (kwa kawaida katika mirija ya fallopian). Hii inaitwa mimba ya ectopic, ambayo ni mimba isiyo ya kawaida na inaweza kuishia katika matibabu ya dharura. Mimba haiwezi kuishi nje ya mji wa mimba uzazi na kwa hali hii inahitaji kutibiwa au kuondolewa kabisa.