Utamfundishaje mtoto wa miaka miwili kushirikiana na wenzake?
Nini utarajie katika umri huu?
Katika umri huu mtoto wako ataonekana mbinafsi sana, atakua mkali pale ambapo mtoto mwenzake atachukua mdoli wake au kupiga kelele kama mgeni atashika mpira wake anaoupenda.
Katika umri huu watoto wengi hawapendi kushiriki na wengine japo anaweza kuwa na rafiki mmoja ambaye anaweza kumpa biskuti yake. Anaweza kucheza na watoto wengine kama utakua karibu yake sana ukimuangalia, lakini tarajia mikwaruzo ya mara kwa mara kati yao. Kushirikiana ni shughuli ya kujifunza hivo itamchukua muda ni vizuri kumuelimisha faida za kushirikiana.
Nini ufanye ili kumsaidia mtoto wako kushiriki?
Mfundishe mchezo wa kupeana vitu
Unaweza kumsaidia mtoto wa kumfundisha michezo ya kupeana mfano mchezo wa kusukuma gari chini na kumpa naye asukume hii itamfanya apende michezo ya kupeana na kuelewa kuwa anapotoa vitu vyake haimaanishi kwamba hatavipata tena, mchukue mdoli wake pendwa na kumbusu kisha mpe naye ambusu.
Usimuadhibu mtoto wako
Kama utamwambia mtoto wako ni mbinafsi au kumuadhibu ili kumlazimisha kushirikiana na wenzake haiwezi kumjenga katika kitendo cha kushirikiana na wenzake. Mshawishi katika njia chanya ili uweze kumjenga kiakili,ili akili yake inapokomaa ajue kushirikiana na rafiki zake ni vema zaidi kuliko kujitenga na vitu vyake.
Zungumza naye
Msaidie mwanao kuelezea hisia zake katika kushirikiana kwa mfano rafiki yake amechukua mdoli wake unaweza kumwambia “sofi anampenda sana mdoli wako anatamani amkumbatie kwa muda” msaidie na yeye kuelezea hisia zake pia, muangalie mtoto wako jinsi atakavyokua mwema anapocheza na wenzake pia muelezee inafurahisha kwa kiasi gani kushirikiana na wenzake.
Mpigishe hatua
Ikiwa kuna watoto wengine wanaocheza naye ni vyema kumwambia mtoto amuweke mbali yule mdoli wake pendwa asijekupotea kisha wahamasishe rafiki zake wanapokuja kucheza kila mmoja aje na vitu vyake vya kuchezea,ili kila mmoja awe na vitu vyake vya kuchezea,na kushirikiana vitu walivyonavo.
Heshimu vitu vya mwanao
Kama mtoto wako atahisi umetoa nguo zake, midoli au kitu chake chochote kwa mtu mwingine anaweza kujisikia vibaya hivyo ni vema kumuomba ruksa na kuheshimu mawazo yake mpe uhuru achague yeye kusema ndio au hapana, hakikisha vitu vyake vinaheshimiwa na kuangaliwa vizuri.
Muongoze kwa mifano
Njia bora zaidi ni kumfundisha kwa mifano mtoto, hivyo shiriki naye “ice cream” yako, mpatie kitambaa chako avae muonyeshe kuvutiwa kuvaa kofia yake, tumia neno kushirikiana ili kuelezea kile unachokifanya. Kitu kikubwa na bora zaidi mfanye aone unavyochukua na kutoa kwa wengine.