Muda mzuri wa kufanya ngono ni kipindi ambacho mwili wako unaruhusu mimba kutungika, ambacho kinadumu mpaka siku sita kwa mwezi. Siku hizi tano zinakupeleka mpaka siku ya kupevuka yai ambayo mwili wako unatoa yai.
Yai lako litaishi kwa siku moja tangu litolewe. Lakini mbegu za kiume zinaweza kuishi mpaka wiki ndani yako hivyo kuna siku sita za mbegu za kiume kusubiri na kukutana na yai.
Una uhakika wa kupata mimba ikiwa utafanya ngono na mwenzi wako ndani ya siku au zaidi ya baada ya kupevushwa yai. Lakini ni ngumu kujua siku sahihi ya kupevushwa yai. Hivyo ni vema kukutana kimwili na mwenzi wako kila siku mbili au tatu na kulifurahia tendo la kumtafuta mtoto.
Kama unataka kuwa na uhakika,itakubidi kufanya mahesabu na kujua lini yai litapevuka ndani ya mwili wako. Yai litapevushwa kulingana na mzunguko wako ambao unategemea:
- Urefu wa mzunguko wa hedhi
- Na kwa kiasi gani hedhi yako ni ya kawaida(regular).
Mzunguko wa hedhi unaweza kuwa mfupi yaani siku 21 au mrefu wa siku 40. Wastani wa urefu wa mzunguko ni karibu siku 28.
Bila kujali urefu au ufupi wa mzunguko wako, kupevushwa kwa yai kunatokea siku ya 14 kabla ya hedhi yako inayofuata kuanza. Ikiwa una mzunguko wa siku 28, kuna uwezekano wa yai lako kupevushwa siku ya katikati ya mzunguko wako. kama una mzunguko mfupi yai linaweza kupevushwa ndani ya siku za mwisho za hedhi yako.
Wanawake wengi wanatofautiana urefu wa mizunguko ya hedhi kwa siku saba. Ikiwa mzunguko wako unatofautiana kati ya mwezi mmoja na mwingine, siku zako za mimba kutungwa zitabadilika pia kwa wiki katikati ya kila hedhi.
Ndo maana ni vizuri kufanya ngono kila siku mbili mpaka tatu kipindi chote cha mzunguko. Ni bora kufanya hivi kuliko kusubiria siku unayofikiri yai litapevushwa. Pia kufanya tendo la ndoa kila siku mbili mpaka tatu huimarisha ubora wa mbegu za kiume.
Nitajuaje yai linapevushwa?
Utaanza kuziona dalili za kuwa kwenye ovulation karibu siku tano kabla ya yai kupevuka. Kujaribu kuelewa mzunguko wako kwa kutumia tarehe za mzunguko wako pekee haitakupa majibu sahihi. Ndio maana kuna umuhimu wa kuelewa na kugundua dalili za mwili wako kipindi upo kwenye “ovulation” ili kufanikiwa kupata ujauzito.
Dalili kuu na ishara vya yai kupevuka vinajumuisha:
- Mabadiliko ya uteute uliopo kwenye mlango wa kizazi.
- Kuongezeka joto la mwili.
- Maumivu ya tumbo.
- Maumivu ya maziwa yanapoguswa
- Kuwa na hamu ya mapenzi kuliko kawaida.
Je, hedhi ambayo inatofautiana mwezi mmoja na mwingine itafanya nipate ugumu kupata ujauzito?
Kuwa na hedhi inayotofautiana mwezi mmoja na mwingi haimaanishi wewe hauna uwezo wa kubeba ujauzito kama wanawake wengine.Lakini kama hedhi yako ikipishana zaidi ya siku 36 ni vema kumuona daktari.
Wakati mwingine, mabadiliko makubwa ya mzunguko wa hedhi yanasababishwa na uvimbe kwenye ovari au shida ya tezi. Hali hizi zinaweza kuathiri nafasi ya kupata ujauzito, hivyo ni vema kupata msaada mapema.
Kadiri mabadiliko ya hedhi yanavyoongezeka ndivyo nafasi ya kupata mimba inapungua. Kwa hiyo fanya mazoezi ya kutafuta na kufuatilia mabadiliko ya uteute kwenye mlango wa kizazi kila siku. Jaribu kufanya tendo la ndoa kila unapogundua uteute kwenye nguo zako za ndani mara mbili au zaidi. Au unaweza kujamiana kila siku katika mzunguko wako.