Je Mtoto Wako Anashiba?

Sheria ya kwanza ya kumnyonyesha mtoto ni kumuangalia na sio kuangalia saa(mda). Kumuwekea mtoto ratiba ya kunyonya kunaweza kuwa hatari katika upatikanaji wa maziwa yako. Lakini kama utamruhusu mtoto wako kuamua muda gani na mara ngapi ananyonya, utakuwa na uhakika mtoto wako anapata maziwa ya kutosha na upatikanaji na usambasazaji wa maziwa yako kuwa imara. Kama mtoto wako amelala kwenye kifua chako upande mmoja wa bega, mbadilishe kuelekea upande mwingine. Ikiwa mtoto wako bado ana njaa, atakula zaidi. Ikiwa hana njaa, jiandae kwa ulishaji ujao.

Ishara zinazoweza kukujulisha mtoto wako anapata maziwa ya kutosha hujumuisha:

Mtoto wako mchanga atanyonya mara 8-12 ndani ya masaa 24.

Mtoto wako anapata choo kila siku baada ya kufikisha siku 4.

Kinyesi cha mtoto wako kinabadilika kutoka nyeusi hadi kijani hadi manjano kadiri anavyokunywa maziwa vizuri (na inapaswa choo kuwa cha njano baada ya siku 4)

Mtoto wako anatakiwa abadilishe nepi 5-6 nzito zilizo loana kila siku baada ya siku ya nne.

Mtoto wako anaongezeka gramu 112 – 196 kwa wiki baada ya kurejesha uzito wa kawaida wa kuzaliwa (kawaida ndani ya siku 10-14).

Watoto wote wana siku ambazo wananyonya sana na siku nyingine ambazo hawanyonyi. Hizi ni tabia za kawaida za unyonyeshaji na sio ishara kwamba kuna kitu sio sawa.

Homoni ya Prolaktini itazalisha maziwa yako. Ikiwa unanyonyesha mara nyingi, kiwango cha homoni ya prolaktini kitaendelea kukaa na kuongezeka kwa wingi. Ikiwa itaongezeka sana na kuwa ya kiwango cha juu, utatengeneza maziwa mengi zaidi na mtoto wako atapata uzito kwa urahisi. Kwa hiyo ni muhimu kuwa unamlisha mara nyingi. Ikiwa unanyonyesha mara kwa mara, kwa muda mrefu, ongezeko la homoni ya prolaktini itashuka. Hivyo ni bora kunyonyesha mara nyingi, yaani mara 8-10 katika masaa 24, na ukitumia karibu dakika 15-45 kwa mlisho mmoja.

Jinsi gani naweza ongeza wingi wa maziwa yangu?

Kutoka kwa maziwa ni njia ya kuongeza utengenezaji wa maziwa. Kama unahisi utokaji wa maziwa ni mdogo kabisa, njia zifuatazo zinaweza kusaidia:

Hakikisha mwanao anatoa maziwa vizuri kutoka kwenye titi lako

Mnyonyeshe kila mara

Badilisha upande kila wakati kila unapomnyonyesha.

Epuka chupa za maziwa, labda kama ni muhimu kwasababu ya matibabu, hakikisha unafikia mahitaji ya mtoto wako kunyonya kutoka kwenye titi lako.

Kamua maziwa na fanya kama ratiba yako, unaweza kukamua maziwa dakika 5-10 kila baada ya kumnyonyesha.

Amka kumnyonyesha au kamua angalau mara moja au mbili usiku.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.