Je, kuna mikao maalumu ya ngono kupata ujauzito kiurahisi?

Je, baadhi ya mikao mingine wakati wa kufanya mapenzi ni bora zaidi kupata mimba?

Unaweza ukawa umesikia baadhi ya mikao kama mwanaume kuwa juu wakati wa kufanya mapenzi, ni bora zaidi ukitaka kupata mimba. Kiukweli hakuna ushaidi wowote kuhusu nadharia hizi. Wataalamu hawajafanya utafiti bado.

Kitu ambacho wataalamu wamefanikiwa kufanya ni kupiga picha na kuonyesha yanayoendelea ndani ya mwili wako wakati tendo linafanyika. Utafiti umeangalizia zaidi mikao ya aina mbili ambayo ni mwanaume akiwa juu na mikao ya kufanya tendo la ndoa kwa kukaa mkao kama mbwa (doggy style) na mwenzi wako kukuingilia kwa nyuma.

Inasemekana njia hizi zinaruhusu kupenya kwa kina kwa uume. Hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa wa kuweka mbegu za kiume karibu na kizazi chako.

Uchunguzi huu wa picha umethibitisha kwamba ncha ya uume hufikia maeneo kati ya kizazi  na kuta za uke katika mikao yote hii miwili. Mkao wa mwanaume kuwa juu ya mwanamke wakati wa kufanya mapenzi unaruhusu uume kufikia eneo mbele ya kizazi. Mkao wa kumuingilia mwanamke kwa nyuma (doggy style) unafikia eneo nyuma ya kizazi.

Je, ninahitaji kufika kileleni kupata mimba?

Ni dhahiri, kwamba ni muhimu sana kwa mpenzi wako kufikia kileleni  ikiwa mnajaribu kupata mtoto. Hakuna ushahidi, hata hivyo, kwamba unahitaji kufika kileleni kupata mimba.

Kwa mwanamke kufika kileleni, jambo la kufurahia na kuridhika. Haina msaada wowote katika kufikisha manii kwenye yai. Mibano milaini ya mji wa mimba inaweza kusaidia mbegu ya kiume kusafiri kwa uhakika, lakini hii hutokea bila hata kufika kileleni

Kwa hiyo, sio muhimu sana kufikia kileleni  ili kupata mimba.

 

Je kuna mikao yeyote inayoweza kutusaidia kuzaa mtoto wa kiume au wa kike?

Hakuna ushaidi, inasemekana  kufanya tendo la ndoa mwanamke kuwa juu itapelekea kuzaa mtoto wa kike, ila mwanaume akiwa juu wakati wat endo hili inapelekea mtoto wa kiume kuzaliwa.

Je, nijilaze baada ya tendo?

Manii yanaweza kukaa ndani ya uke wako na maeneo ya karibu na kizazi zaidi kuliko ukinyanyuka mara baada ya tendo. Hata hivyo, mamilioni ya manii hutolewa na kiungo kimoja cha mwanaume, hivyo basi lazima ziwe nyingi katika uke wako hata ukisimama mara tu baada ya tendo.

Kama una muda wa kutosha, ni vema kukaa kitandani mpaka baada ya nusus saa baada ya kufanya mapenzi. Jaribu kulala kwa mgongo, na mapaja yako yakiwa yamenyanyuliwa juu yam to ili kuhimiza manii kusafiri kwa wepesi kwenda kwenye yai. Usijaribu kufanya hivi kama mshauri wako wa afya alikushauri ukojoe mara baada ya kufanya tendo.

Ujanja mwingine kwa wanawake ni kulala kwa mgongo na kuchochea(cycling) miguu yako juu kwa dakika chache baada ya tendo.

Jambo la muhimu la kukumbuka ukiwa unajaribu kupata mimba, ni kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara inaweza kusaidia. Kufanya tendo kila siku mbili mpaka tatu inaongeza nafasi ya kupata mimba ndani ya mwaka, ukilinganisha na kufanya mapenzi mara moja tu kwa wiki.

Ikiwa umejaribu kupata mtoto  kwa mwaka au zaidi bila mafanikio, muone mshauri wako wa afya. Ikiwa wewe una umri wa miaka 36 au zaidi au hauna hedhi ya  kawaida, unaweza kufanya miadi hata mapema.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.