Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Mwezi 1

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

  • Atanyanyua kichwa chake ukimlaza tumboni kwako.
  • Ana mwitikio katika sauti atakayosikia.
  • Kuzitambua sura na kushangaa.
  • Ataona rangi nyeusi na nyeupe.
  • Anageuza kichwa kuelekea mwanga unapotokea.

 

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Anafuata muelekeo wa vitu.
  • Anatoa sauti za “ooh” na “ah’’.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Kucheka
  • Kunyanyua kichwa digrii 45.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.