Hongera! Mtoto wako sasa si kichanga tena, na ametimiza mwaka mmoja.
Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Anaigiza kazi za watu wengine kama kupika,kuongea na simu-mara nyingi anaigiza kile alichoona wewe na mwezi wako mnafanya.
- Kupiga makofi, kuaga na kuonyesha kitu kwa kidole.
- Kutumia ishara muhimu kama kutikisa kichwa akisema hapana au kupungia mkono akiaga.
Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)
- Kuitikia na kuelewa maswali rahisi utakayomuuliza na uelekeo mfano: njoo hapa.
- Atasema maneno kama “mama” au “baba” na mishangao kama”aaah, ooho”
- Mtoto ataanza kutembea hatua chache bila kushikwa na mtu.
- Kusimama mwenyewe.
- Wanatambua vitu na kukiangalia mara utakapokitaja.
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Kutembea vizuri
- Kutumia vitu sawa kama kunywa maji kutumia kikombe, kuchana nywele kwa chanuo.
- Mtoto kuelewa maneno kama kunywa, gari au mpira.
- Anasema maneno mengine mawili ukiachana na mama na baba.