Hisia za mtoto zitaanza kukua, anaweza kuanza kutumia milio tofauti wakati wa kulia ili kukujulisha nini anataka (anahisi) na kugeuza kichwa chake upande wa pili kuonyesha amechoshwa.
Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Anaweza kutofautisha sura yako na sura za wengine.
- Ataanza kugeuza kichwa upande wa pili kuonyesha kuchoka au kukerwa na jambo.
- Atafuatilia kitu kinachosogea kwa macho yake.
Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)
- Kulia tofauti kwa hitaji tofauti-njaa, kubadilishwa nepi, maumivu n.k.
- Atafungua na kufunga mikono yake.
- Atafurahi kucheza na watu wengine, atalia pale mtu atakapoacha kucheza nae.
- Mtoto atagundua sauti yako.
- Atatengeza viputo na mate yake na kupasua.
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Kugeuza kichwa upande sauti inapotokea
- Kujiviringisha na kulala na mgongo kama ulimlaza kwa tumbo.
- Kutanisha mikono yake na kushika mdoli.