Kuwasha, kuvuta kwa chuchu
Kadiri homoni za mimba zinavyoongeza usafirishaji wa wa damu kwenye matiti yako unaongezeka, hivyo unaweza kuhisi hali ya kuvuta kuzunguka chuchu zako.
Hii inaweza kuwa moja ya dalili za awali za mimba, na muda mwingine kugundulika pia ndani ya wiki au zaidi ya baada ya mimba kutungwa. Mara baada ya mwili wako kuzoea ongezeko la homoni, hali hii itapotea.
Maumivu ya tumbo na kuona matone ya damu kwenye nguo za ndani.
Sio kawaida kuchafuka ukiwa karibia wiki 6 za ujauzito. Unaweza kugundua rangi ya pinki kwa mbali au madoa ya kahawia katika nguo zako za ndani(chupi) au wakati unakojoa au kuhisi maumivu ya tumbo kwa mbali. Wataalamu hawana uhakika kabisa kwanini dalili hizi zinatokea katika hatua za awali za mimba. Inasadikika ni kwasababu ya ukuaji wa plasenta.
Kama umekumbwa na tatizo la kutokwa damu ambalo sio kawaida, muone daktari mapema ili kuwa katika hali ya usalama.
Kujisikia kuumwa
Kama una bahati utaepuka kichefuchefu kabisa. Hata hivyo,magonjwa ya asubuhi ni moja ya dalili za awali za kawaida za mimba, dalili hizi zinaweza kuanza mapema katika wiki ya nne. Unaweza kujisikia kuumwa na kichefuchefu. Hali hii inaweza kukupata mda wowote ndani ya siku, mchana au usiku.
Kukua,kuvimba kwa matiti
Mara baada ya kufika wiki ya sita ya ujauzito wako, matiti yako yanakua nyeti zaidi. Inakua sawa na jinsi unavyojisikia kabla ya hedhi.
Unaweza kugundua kwamba maziwa yako yamekua na kuvimba,na mishipa kuonekana chini ya ngozi. Kukua kwa maziwa ni dalili ya kawaida katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba.
Kujisika kuchoka
Umechoka?Unaweza kushinda kitandani mda wote kadiri mwili wako unavyojitahidi kukubaliana na uwepo wa mtoto ndani yako, tangu mwanzo wa mimba. Homoni za mimba za mwili wako ndio zinakufanya kuhisi umechoka, mwenye hasira na hisia kali.
Uchovu ni dalili ya kawaida ya mimba, na hutokea zaidi katika kipindi cha kwanza cha mimba na hatua za mwisho za ujauzito.
Kupata haja ndogo mara kwa mara
Katika wiki yako ya sita ya mimba utagundua unakojoa sana. Hii ni kwasababu ya mjumuiko wa homoni za mimba, wingi wa damu ndani ya mfumo wako na figo zako kufanya kazi nzito zaidi. Ikiwa utahisi maumivu au kuungua wakati unakojoa, unaweza ukawa na UTI, muone daktari kama unahisi umepata maambukizo ya ugonjwa huu.
Chuchu nyeusi
Mabadiliko ya ngozi ni ya kawaida wakati wa ujauzito. Moja ya mabadiliko ya kwanza ambayo unaweza kuona ni mduara wa ngozi pande zote za chuchu zako (vidogo) unakua mweusi. Hii inaweza kutokea kuanzia wiki ya nane.
Unaweza pia kugundua kwamba viuvimbe vidogo vya ngozi vinavyozunguka chuchu zako vinajitokeza zaidi na kuchomoza zaidi. Uke wako pia unaweza kubadilika rangi na kuwa rangi ya pinki ya kukolea ingawa unaweza usitambue
Hamu ya kula kubadilika na hata hisia ya harufu hubadilika
Hamu ya kula inaweza ikawa ni moja ya dalili za mimba/ujauzito. Unaweza kuachana na aina flani za chakula mwanzoni hata kabla hujakosa siku zako.
Utaanza kutambua hisia ya chuma mdomoni, au kutambua hupati hamu ya kunywa ya kahawa, au chakula ambacho umezoea kula.
Kukosa hedhi
Ikiwa hedhi yako ni ya kawaida, na imechelewa kuanza, ni bora ukachukua kipimo cha mimba kabla hujagundua dalili nyingine. Kukosa hedhi ni moja ya ishara hakika ya ujauzito.Lakini ikiwa hedhi yako si ya kawaida au umepoteza uelekeo lini hedhi yako inatarajia kuanza,unaweza usigundue kama hedhi imechelewa. Katika wakati huo matiti yanakua, kichefuchefu na kwenda haja ndogo kila mara zinweza kuwa dalili za mwanzo kuonyesha wewe ni mjamzito.
Kipimo cha nyumbani cha mimba
Vipimo vingi vya mimba vya nyumbani vitakupatia majibu ya uhakika , kama ukisubiri mpaka siku ya kwanza ya kukosa hedhi yako.