Moja ya sababu inayoleta matatizo ya kuzaa pale umri unapokua mkubwa ni kupevushwa yai mara chache kuliko kawaida. Kadiri wanawake wanapoendelea kukua mizunguko yao ya hedhi inaanza kubadilika na mayai kushindwa kupevushwa kwa wakati. Idadi ya mayai na ubora wa mayai unapungua, mwanamke anapofika umri kati ya miaka 30 mpaka 40. Utafiti unaonyesha ubora wa mayai unaweza kuongezwa ihali idadi yake haiwezi kuongezeka. Virutubisho vya “myo-inositol”, asidi ya foliki na “melatonin” vimeonyesha kuongeza ubora wa mayai na kazi za mfuko wa mayai.
Sababu nyingine zinazofanya kupata ujauzito baada ya miaka 35 kuwa vigumu ni pamoja na:
- Maambukizi au upasuaji uliosababisha kovu kwenye tishu maeneo yanayozunguka mfuko wa mimba,mirija ya falopiani au mlango wa kizazi cha mwanamke.
- Ugonjwa wa “endometriosis”.
- Uvimbe katika mfuko wa uzazi.
- Upungufu wa uteute ndani ya mlango wa kizazi.
- Magonjwa ya kudumu/sugu kama shinikizo la damu au kisukari.
Kuharibika mimba pia ni tatizo kubwa kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35. Hii inasababishwa na ongezeko la mabadiliko ya jenetiki za uumbaji. Wanawake wenye umri kati ya miaka 35-45 wana nafasi kati ya asilimia 20-35 ya mimba kuharibika
Ni nini nifanye niongeze nafasi ya kuzaa baada ya umri wa miaka 35?
Kujaribu kujifungua baada ya miaka 35 linaweza kuwa jambo la kuelemea, lakini kuna mambo mengi ya kufanya kukusaidia kushika ujauzito haraka.Yafuatayo ni mambo ya kukumbuka:
- Andaa ratiba ya kuonana na mtaalamu wa uzazi – wewe pamoja na mshauri wako wa afya mnaweza kupitia historia ya matibabu yako, matibabu ya sasa na maisha yako kwa ujumla. Kwa kufanya hivi, kunasaidia kuyagundua matitizo na wasiwasi wowote hasa unapojiandaa kupata ujauzito baada ya miaka 35.
- Wanawake wenye umri mkubwa wanachukua mda kupata ujauzito – kuwa na imani pale unapochelewa kupata ujauzito, kumbuka wastani wa namba ya kupata ujauzito kwa wanandoa walio na umri zaidi ya mika 35 ni 1-2 kwa mwaka.
- Mwanamke aliye na afya kimwili,kiakili na kihisia anaweza kupata ujauzito – pombe,sigara na matumizi ya kahawa(vinywaji vyenye kafeni) zinaweza kupunguza nafasi ya wewe kupata ujauzito. Pia kuwa na uzito mdogo au mkubwa sana inaweza kuingilia ufanyaji kazi wa homoni.
- Angalia ishara za mwili wako zitakazo kusaidia kujua wakati gani ni wa kufanya ngono ili kupata ujauzito – rekodi jotoridi la mwili na majimaji ukeni ili kujua muda muafaka wa kufanya ngono. Ishara hizi zitakusaidia kujua ni wakati gani yai linapevushwa ndani ya mwili wako na kama yai lako linapevushwa kwa wakati.
- Mtembele mshauri wako wa afya kama hujafanikiwa kupata ujauzito baada ya miezi sita ya kufanya ngono – Kutana na mshauri wako wa afya kujadili uwezekano wa kupima uwezo wako wa kupata ujauzito. Kwa wakati huu unaweza kumtembelea mtaalamu wa maswala ya uzazi.
Tumia kirutubisho chenye myo-inositol (virutubisho vinavyotumika kutibu watu wenye uvimbe kwenye mfuko wa mayai) kukusaidia kuboresha mayai yako.