Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 3

Hatua mwanao alizofuzu(watoto wengi wanazifikia)

  • Anaweza kuongea na kueleweka mara nyingi.
  • Anaweza kuvaa nguo mwenyewe.
  • Anaruka.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Atasaidia kurudisha midoli yake baada ya kumaliza kucheza
  • Anapanga vitu kwa makundi
  • Anajua kutumia maneno ya wingi.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Kusimama na mguu mmoja
  • Kutatua mitihani(mafumbo) na vitendawili  katika midoli yake anayochezea
  • Anaweza kuimba nyimbo za watoto alizosikia katika simu yako au kipindi cha watoto.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.