Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Anaweza kufanya shughuli nyepesi ulizompa afanye kama kukusanya midoli yake na kurudisha kwenye boksi la kutunzia.
- Anaonyesha kutaka usikivu kutoka kwako.
- Anaweza kuvua nguo
Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)
- Anaweza kunawa mikono ila atahitaji msaada wako kumkausha
- Anaweza kufungua mifuniko ya makopo kwa kuzungusha
- Anaweza kusugua meno kwa msaada wako
- Anaweza kuvaa nguo
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Kuongea fasaha wakati mwingi
- Kuchora mstari kwa ulalo au kusimama
- Kutumia mkasi