Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Anaweza kutaja angalau sehemu sita za mwili wake
- Nusu ya maelezo yake yanaeleweka
- Anaweza kutengeeza sentensi fupi fupi
Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)
- Ataanza kujielezea
- Kupanga vitu kwa makundi
- Kushuka ngazi
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Kuelewa dhana ya baadae na sasa hivi.
- Kuelewa tofauti ya jinsia.
- Anajifunza kuruka.