Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Ataigiza kumlisha mdoli
- Anaweza kuvua nguo zake ukimsaidia
- Atatupa uchafu kwenye ndoo ya uchafu akikuiga wewe au mtu mwingine aliyemuona anafanya hivyo.
Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)
- Anajifunza maneno mengi, kumi au zaidi kwa siku.
- Anaweza kupanda ngazi lakini si rahisi kushuka.
- Anatafuta vitu ulivyoficha ambavyo awali alikua anaviona.
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Anaanza kuchunguza sehemu zake za siri.
- Anaweza kutaja majina ya sehemu nyingi za mwili wake.