Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Mwaka 1 na Miezi 7

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

  • Anaweza kutumia kijiko na uma
  • Anaweza kukimbia
  • Anaweza kurusha mpira

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Nusu ya maelezo yake yanaweza kueleweka.
  • Atagundua kama amekosea kitu kama kumuita dada wa nyumbani mama au kumuita paka mbwa.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Kunawa mikono na kusugua meno kwa msaada wako.
  • Kunyooshea kidole ukitaja kitu kama mbwa, kikombe.
  • Anajua anapohitaji kujisaidia

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.