Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Mwaka 1 na Miezi 4

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

  • Anaweza kufungua kurasa za kitabu
  • Anakasirika na kuonyesha hasira pale anaovunjika moyo
  • Anapendelea midoli milaini au kitu chochote kilaini

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Atagundua raha ya kupanda vitu kama ukuta, kabati na juu ya meza
  • Atajifunza njia sahihi ya kutumia vitu mfano simu

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Anavua baadhi ya nguo mwenyewe
  • Anachezea chakula sana
  • Atabadilika na kulala mara moja mchana badala ya mbili

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.