Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Mwaka 1 na Miezi 2

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

  • Anaweza kula chakula mwenyewe( matunda yaliyokatwa kidogokidogo).
  • Anaiga wengine.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Kutembea mwenyewe vizuri.
  • Anaweza kuanzisha mchezo.
  • Ataweza kuonyesha kiungo chochote cha mwili wake unapokitaja.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Kutumia kijiko au uma.
  • Anaweza kufananisha mfuniko wa ndoo au sufuria na ndoo yenyewe au sufuria yake.
  • Anasukuma na kuvuta midoli yake akiwa anatembea.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.