Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Anatambaa vizuri
- Anazunguka na kuchunguza sana
- Mtoto ataanza kuchunguza vitu katika njia tofauti kama kugongagonga, kutupa na kutikisa
Hatua za ukuaji zinazojitokeza(nusu ya watoto wanazifikia)
- Anasema mama au baba.
- Ananyooshea mkono vitu vilivyo mabali.
- Anaitikia ukimwita na anaelewa maana ya neno HAPANA.
- Anaonyesha anachotaka kwa kuonyesha ishara.
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Anaweza kutumia kikombe mwenyewe.
- Kusimama mwenyewe kwa sekunde chache.
- Ataanza kujilisha mwenyewe baadhi ya vyakula kama matunda yaliyokatwa vizuri.