Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 4

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

  • Anavutiwa na mfumo wa vitu.
  • Anataka kushika kila kitu na kuweka mdomoni.
  • Ameanza kulia kwa sauti nyororo.
  • Anajitahidi kupata usikivu wako
  • Ataigiza baadhi ya sura utakazomuonyesha

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Mwanao ataanza kujiviringisha,kuwa makini usimuache kitandani mwenyewe.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Kuota jino lake la kwanza
  • Kushika chupa yake ukiwa unamlisha.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.