Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)
- Anaanza kutoa sauti, milio ya kitoto na minong’ono.
- Ataanza kufuatilia vitu kwa macho na kuwagundua watu aliowazoea kwa mbali.
- Anagundua mkono wake.
- Atanyanyua kichwa chake juu kwa muda mfupi.
Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)
- Kutabasamu,kucheka
- Kuinua kichwa digrii 45.
- Kusogeza miguu na mikono taratibu.
Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)
- Kujiinua unapomlaza tumboni kwako.
- Kuhimili uzito wake kwenye miguu yake
- Kukihimili kichwa chake kwa uimara
- Atajibembeleza mwenyewe kwa kuweka mkono mdomoni.
Ataanza kunung’unika na kusumbua pale anapochoshwa na kitu au mdoli.