Zifahamu Dalili za Ujauzito wa Mapacha

Mambo gani yanaongeza nafasi ya kupata ujauzito wa mapacha.

Jenetiki (vinasaba)  ni jambo la muhimu litakalo kuwezesha kupata watoto mapacha, nyinginezo ni kama vile;

  • Watoto wa kupandikizwa, ni njia ya kitaalamu inayofanyika pamoja na njia nyingine za uzazi kama vile IVF (in vitro fertilization) ambapo zaidi ya yai moja la mwanamke huwekwa kwenye mfuko wa uzazi, ambapo huongeza nafasi ya kupata mapacha.
  • Baada ya miaka 30 mwili wa mwanamke huzidisha utoaji wa homoni FSH (follicle stimulating hormone) ambayo husababisha kuachiliwa zaidi ya yai moja kwenye mfuko wa kizazi ambayo pia huchangia kuleta mapacha.
  • Kama umepita urefu wa kawaida na BMI yako ni 30 au zaidi nafasi ya kupata mapacha huongezeka.
  • Kama tayari wewe ni mama wa mapacha basi una nafasi ya kupata mapacha tena.
  • Utafiti wa madktari umeonyesha wamama wasiotumia nyama wana nafasi kubwa ya kupata mapacha. Kupungua kwa kiwango cha mapacha miaka ya 1990 ilisababishwa na matumizi ya madawa ya kukuzia ng’ombe kwa ajili ya maziwa na nyama.

Wanawake wa kinaigeria wana nafasi kubwa sana ya kupata mapacha kutokana na kula mazao kama mihogo na viazi. Kama haupo kwenye nafasi yoyote iliyotajwa hapo juu bado una nafasi ya kupata mapacha.

Utajuaje kama umepata ujauzito wa mapacha?.

  • Kiwango cha juu cha homoni, ambayo husababisha kuongezeka kwa kiwango cha magonjwa ya asubuhi katika kipindi cha wiki mbili za kwanza za ujauzito wakati mwingine unaweza kupata ugonjwa wa asubuhi kujulikana kama “hyperemesis gravidarum” na pia kichefuchefu.
  • Ujauzito wa mapacha unaleta uchovu sana, kulala, na kujisikia vibaya, wiki mbili au tatu za mwanzo za ujauzito. Kulisha watoto wawili inahitaji usingizi wa kutosha na chakula bora kwa ajili ya mwili wako ili uweze kufanya kazi vizuri.
  • Hamu ya kula inaongezeka, kwani mwili wako unahitaji chakula cha kutosha kwa ajili ya kukuza watoto vizuri
  • Mfuko wa uzazi huwa mkubwa kwasababu umebeba zaidi ya kiumbe kimoja,hii inasababisha tumbo kuwa kubwa.
  • Mabadiliko ya jinsi unavyojisikia ni kitu cha kawaida kwasababu kiwango cha homoni kinaongezeka ili kuweza kustaimili ukuaji na maendeleo ya watoto, hali hii inaonekana sana wiki sita tangu ujauzito.
  • Ujauzito hutambilika sana baada ya kipimo cha mkojo au damu,baada ya kipimo hichi unaweza kupata uhakika kama una ujauzito wa kawaida au wa mapacha. Vilevile ujauzito wa mapacha unapelekea kuwa na mstari tumboni wenye rangi iliyokolea.

Tukiachana na hizo kuna ishara nyingine ambazo zinatofautisha ujauzito wa kawaida na ule wa mapacha.

Ishara zaidi za ujauzito wa mapacha

Kulingana na ishara za mwanzounaweza kutambua kama una ujauzito wa mapacha .lakini kuna ishara zaidi zinazoweza kukupa muafaka zaidi:

  • Wakati una ujauzito wa mapacha unaweza kuongezeka uzito haraka sana kuliko kubeba mtoto mmoja tu.
  • Uchunguzi wa mara kwa mara wa daktari wako unaweza kukusaidia kujua umri wa mtoto na ukuaji wake, kama kipimo hiko kinaongezeka kwa sentimita moja kila wiki basi ni ishara moja kuwa unatarajia kupata mapacha.
  • Kusogea kwa mtoto tumboni hutokea mapema sana wakati ukiwa na ujauzito mapacha kuliko mtoto ule wa mmoja.
  • Kuelekea mwisho wa miezi mitatu ya kwanza, daktari anaweza kuchukua kipimo kiitwacho “Doppler heartbeat count” kuweza kutambua mapigo ya moyo ya mtoto. Kama umebeba mapacha utasikia mapigo ya moyo mara mbili.
  • Ujauzito wa mapacha huambatana sana na kukosa pumzi, hii ni kwasababu ya ukuaji wa mfuko wa uzazi unaobana mapafu hivyo kusababisha kukosa hewa.
  • Nyonga kuuma ni ishara mojawapo ya ujauzito wa mapacha kwani kukua kwa mfuko wa kizazi kusio kwa kawaida husababisha nyonga kuuma kwani uzito unaongezeka na kukandamiza nyonga.
  • Maumivu ya uzazi ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito wa mapacha na unahitaji uangalizi wa madaktari kwa haraka.
  • Maumivu ya mara kwa mara ya mgongo ni ishara ya kuongezeka uzito kwa haraka, na kuongezeka kwa homoni ndani ya mwili. Kusimama wima na kuweka kifua mbele huweza kusaidia kukufanya upumzike vyema. Na kuvaa viatu visivyo na soli ndefu pia husaidia, wakati mwingine epuka kukunja magoti kwa muda mrefu wakati wa kukaa.
  • Kupata haja ndogo mara kwa mara, ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito. Lakini wakati una ujauzito wa mapacha haja ndogo inaongezeka zaidi kwasababu mfuko wa uzazi unakandamiza kibofu cha mkojo hivyo kusababisha kupata haja ndogo mara kwa mara.  Ni vizuri pia kupata haja kubwa, hakikisha unakula vyakula laini na vimiminika vya kutosha.
  • Kuongezeka kwa mapigoya moyo ni jambo lingine linaloweza kukupa uhakika kwamba unatarajia mapacha. Ongezeko la damu kwenye mwili linaweza likawa moja ya sababu.
  • Mwili wako unahifadhi maji mara mbili zaidi wakati ujauzito wa kawaida, ambayo yanakusaidia kuepuka tatizo la “edema”. Maji yanahifadhiwa mwilini ili kurudishia yale yaliotoka. Matunda kama matikiti maji, tofaa, machungwa, mapeasi na mananasi yanasaidia kuhakikisha mwili una maji ya kutosha. Acha kuvuta sigara na hakikisha ulaji wa chumvi ni wa kiwango kidogo.
  • Uchunguzi wa “Alpha fetoprotein test (APF)” unaofanyika baada ya miezi sita kuhakikisha kiwango cha protini kinatolewa na kijusi kwenye maini yake. Kiwango cha tofauti cha APF kinaweza kuonyesha uwepo wa mapacha kwasababu kitaongezeka mara mbili.

Tukiachana na hayo kuna ishara nyingine za kuonyesha uwepo wa mapacha ambazo ni sawa na ujauzito wa kawaida.

  • Harufu ya baadhi ya vyakula itakuchefu na kukufanya usikie kichefuchefu.
  • Ujauzito wa mapacha unahitaji mzunguko mwingi wa damu kuhakikisha ukuaji bora wa watoto, ongezeko la damu husababisha shinikizo la damu kuongezeka hasa katika mishipa ya damu ya miguu ijulikanayo kama “varicose veins”. Hatahivyo mkandamizo wa mtoto katika mfuko wa uzazi unaongeza upana wa mishipa hasa ile ya kizazi.
  • Matatizo ya mmeng’enyo wa chakula kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, kiungulia nk. Epuka vyakula vyenye viungo,mafuta mengi na kunywa maji yakutosha, pia kula kidogokidogo kwa mara nyingi uwezavyo.
  • Kukosa usingizi ni kitu cha kawaida sana hasa ukiwa na maumivu ya mgongo, nyonga kukata,kichefuchefu na kuchoka. Kulala kwa ubavu na kuweka mto katikati ya miguu yako na tumbo lako.
  • Katika wiki ya nne mpaka ya tano ya ujauzito wa mapacha unaweza kuwa na matiti yanayowasha na kuuma. Hii ni kwasababu ya mabadiliko ya homoni ndani ya mwii wako mpaka wiki ya sita, chuchu nazo huzidi kuwa nyeusi na kuuma pia, kuvaa sidiria za uzazi zinaweza kusaidia kupunguza maumivu.
  • Ujauzito wa mapacha unaweza kuongeza zaidi uwezekano wa kupata msongo wa mawazo baada ya kujifungua. Kwasababui inamchukua mama muda mrefu zaidi kubadili ratiba baada ya kujifungua. Tofauti na ujauzito wa kawaida mama wa mapacha anachoka zaidi kwasababu inambidi awalishe zaidi. Mazoezi kidogo na mapumziko yakutosha huweza kusaidia katika kipindi hiki. Unaweza kuongea na wazazi wengine juu ya taratibu na mambo gani yafanyike kutoka kwenye ujuzi walionao kwenye uzazi wa mapacha.

Tumbo kubwa ni ishara ya ujauzito wa mapacha. Lakini haimaanishi kwamba unatakiwa kuongezeka kilo kuliko ujauzito wa kawaida.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.