Dalili za mwanzo ni kutoka damu kwa wingi, maumivu makali na tumbo kukaza. Kutokwa damu kunaweza kutofautiana na kawaida maana damu inakuwa nyekundu mpauko.
Damu huweza kutoka kwa siku kadhaa mfululizo, inaweza kuwa ngumu kutambua kinachoendelea, mimba kuharibika inaweza kuleta upweke wa hali ya juu, hasira, woga na kujiskia vibaya.
Kama damu inatoka kwa matone tu au nyepesi,kumbuka ni jambo la kawaida kutoka damu kipindi cha mwanzo cha ujauzito hivyo usiwe na wasiwasi sana lakini wasiliana na mshauri wako wa afya.
Nifanye nini kama nadhani mimba imeharibika?
Kama una dalili za mimba kuharibika piga simu hospitali. Mwone daktari wa wanawake, au hata kwa njia ya simu anaweza kukupa ushauri.
Kama una mimba chini ya miezi sita unaweza kushauriwa kubaki nyumbani tu na kuona nini kitatokea.
Kama mimba yako ina miezi zaidi ya sita,unashauriwa uwahi hospitali ili kufanya kipimo cha “ultrasound” na vipimo vingine zaidi. Mtaalam anaweza kukupa kipimo kupitia njia ya uzazi, njia hii ya kipimo inaweza kutoa matokeo mazuri ya mfuko wa uzazi na ni salama kabisa. Na hakuna madhara yoyote.
Vipimo hivi vitaangalia afya yako na kukupa majibu kamili kama umepoteza ujauzito au ujauzito ni salama. Daktari anaweza kusema kama mimba itaharibika , iliharibika au imeharibika baada ya kuangalia matokeo ya vipimo.
Baada ya uchunguzi utaambiwa uende nyumbani kupumzika na hospitali watakupa namba ya simu masaa 24 utakayopiga kama kutakua na mabadiliko yoyote.
Utahitaji msaada mzuri wa taulo safi na vitambaa vya usafi au pedi za usiku ili kufyonza damu yeyote. Usitumie pedi za kuingiza ndani ya uke-kisodo (tampons) maana zinaongeza nafasi ya maambukizi. Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu kama paracetamol. Ikiwa daktari wako au mshauri wako wa afya amethibitisha mimba yako imeharibika unaweza kutumia ibuprofen pia. Ni vema kumuomba mwenza wako au rafiki yako akununulie haya mahitaji kama hauna ndani kwako.
Kuweka chupa ya maji vuguvugu huweza kupunguza maumivu ya tumbo, kama huwezi kuvumilia maumivu ya tumbo unaweza kumpigia simu daktari wako.
Naweza kufanya lolote kuzuia damu kutoka?
Pindi mimba inapoharibika hakuna kitakachoweza kufanyika kuzuia. Kulala kitandani ni muhimu.
Damu kupungua kutoka au kuacha, inaweza kukustaajabisha. Ukweli ni kwamba damu inaganda kwenye mlango wa kizazi na kuendelea kutoka kama mabonge ukisimama au ukienda uwani.
Nini kinatokea baada?
Ni jambo tu la kuupa mwili wako nafasi ya kupumzika, na kutegemea kwamba mwenzi wako atakua yuko na wewe kukufariji na kuzingatia kuwa unaendelea vizuri.
Kama damu imepungua kutoka na hauna maumivu, unaweza kupumzika tu nyumbani. Na endelea kuwasiliana na daktari wako ukimjulisha nini kinaendelea.
Kama mwenzi wako hataweza kuwa na wewe kila wakati, pengine mtu mwingine wa karibu anaweza kuwa karibu na wewe. Kwasababu kupoteza mtoto kabla hajazaliwa inaweza kuambatana na matatizo. Kama utapata tatizo lolote kati ya haya unaweza kuwasiliana na daktari wako.
- Kutokwa damu kunazidi na kunaloanisha zaidi ya pedi moja ya uzazi ndani ya lisaa limoja, au kutokujiskia vizuri, au kuzimia na kushindwa kuendelea kuvumilia kutokwa na damu, hii ina maana unapoteza damu sana.
- Kuwa na maumivu upande mmoja na kuhisi ganzi katika tumbo lako, nyonga au mabega, kusikia kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio, au kuwa na maumivu ukienda msalani. Hizi zote ni ishara za mimba kutungwa nje ya mfuko wa mimba ambayo inahitaji matibabu haraka ili kulinda afya yako.
- Unahisi homa na kutokujiskia vizuri kiujumla, kama vile una mafua, na maumivu ya tumbo yasioisha hizi zote ni ishara za kupata maambukizi.
Kwa muda gani damu hutoka baada ya mimba kuharibika?
Kutokwa na damu huchukua wiki moja mpaka wiki mbili damu inakua imeacha kutoka. Hata hivyo wiki moja au mbili zinaweza zikapita na na pia ikabidi uendelee kujihudumia unavyoendelea kupata nafuu kimwili na kiakili.
Kama damu haijaacha kutoka ndani ya wiki mbili wasiliana na daktari wako haraka iwezekanavyo
Kuendelea kutokwa na damu inaweza kumaanisha una vipande vya tishu ndani ya mfuko wa uzazi, wakati mwingine kutokwa damu kunaweza kusababishwa na maambukizi ulioyapata ndani ya mfuko wa uzazi, inapaswa kuendelea na matibabu ili kupata nafuu.
Nifanye nini nipate nafuu baadaye?
Kama umepata nafuu baada ya mimba kuharibika au unahitaji matibabu zaidi, wewe na mwenzi wako mnapaswa kuwa pamoja na msiruhusu huzuni kuchukua nafasi.
Kama unaendelea kujiuguza nyumbani, unaweza ukahisi unataka kujishughulisha baada ya siku chache, utahitaji siku chache bila kazi, ingawa unaweza kuwasiliana au kumwona daktari wako ili kupata ruhusa ya kupumzika utakayo mpatia mwajiri wako.
Daktari wako anaweza kukupa miadi kama utahitaji,na pia unaweza kufanya vipimo zaidi kuhakiki kuwa hali yako iko sawa.