Njia za Kumdhibiti Mtoto Katika Matumizi ya Simu na Luninga

Sio sahihi kumuhamasisha mwanao katika matumizi ya simu na kompyuta katika umri wake lakini luninga ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Hivyo zifuatazo ni njia saba za matumizi sahihi ya luninga na simu:

 

Usimshawishi mwanao katika matumizi ya simu, komputa na luninga ikiwa haonyeshi kuvutiwa navyo

Asichokifahamu mtoto hawezi kukihitaji, hivyo kama hajaonyesha kuvutiwa na simu na kompyuta hakuna sababu ya kumshawishi. Subiri hadi pale atakapoonyesha kutambua na kuvutiwa na vitu hivi kabla hujamtambulisha.

 

Kikomo cha matumizi ya simu, komputa na luninga

Weka kikomo katika mda wa kukaa katika luninga, simu au kompyuta, isiwe zaidi ya dakika 20. Mtoto wako anahitaji mda wa masaa 3 kuwa makini kwa siku ili aweze kukua vizuri. Unapotumia muda mwingi katika luninga mtoto wako atashindwa kuyajua mazingira yanayomzunguka kwa kutembea, kukimbia na kuruka.

 

Weka muda wa kutazama luninga kwa pamoja

Tazama luninga au simu na mwanao huku ukimuelezea na kucheza kwa pamoja. Hii inaweza kumsaidia kama vile ukiwa unasoma kitabu, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa misamiati na uwezo wake wa kutunza kumbukumbu. Pia atapata muda mzuri wa kufurahi na wazazi wake.

 

Chagua michezo sahihi kwa mtoto kwa kuzingatia umri wake

Zingatia michezo ambayo inamsaidia mtoto chini ya miaka mitatu. Michezo hiyo:

  • Iwe na uwiano sawa na umri wa mwanao.
  • Imfanye mwanao acheke
  • Impe mwanao malengo ya kufanikisha.
  • Iwasisitize wazazi kushiriki.

 

Zingatia zaidi michezo si kujifunza

Mtoto wako anatakiwa kuona luninga au simu kama moja kati ya midoli yake. Usijaribu kutumia simu na luninga kama sehemu ya kumfundisha mtoto wa mwaka mmoja kuhusu herufi na kuhesabu. Hakuna ushahidi kuwa michezo ya kompyuta au shughuli nyingine za mtandaoni zina manufaa ya kielimu kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili.

Kinyume na hapo, nenda kwenye michezo na shughuli ambazo kiujumla zitamsaidia mtoto kujenga uwezo wa kujifunza kwa haraka. Inaweza kuhusisha kusikiliza wimbo mzuri na kuelewa chanzo na athari, kinyume cha vitu, rangi na utambuzi wa maumbo. Mtoto wako atakua na uwezo mzuri wa kujifunza ikiwa ni hadithi, wimbo au mchezo mzuri.

 

Chagua michezo yenye picha ambayo ni rahisi kuona

Usitarajie mtoto wako kuiga picha zaidi ya moja katika luninga au simu. Itakuwa vigumu mwanao kuelewa na kufurahia michezo au hadithi zinazoonyeshwa sehemu yeney watu wengi kama sinema.

 

Chagua michezo yenye nyimbo nyepesi

Tangu kuzaliwa watoto wanapenda sana nyimbo na sauti za mashairi na uimbaji wa nyimbo. Na hadi wanapokua na umri wa mwaka kurudiarudia nyimbo inawasaidia watoto kuelewa maneno. Pia wanaweza kuanza kujifunza kuhusu kifuatacho.

Kama mtoto wako amefikia umri wa miezi 18, cheza naye kwa kutengeneza sauti za mlio wa kengele na saa, mtoto wa umri huu anapendelea sana hivyo.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.