Mlo Kamili kwa Mtoto ni Upi?

Mlo kamili ni nini na kwanini mlo kamili ni muhimu?

Mlo kamili unajumuisha vyakula vingi tofauti, utakao msadia mtoto kupata mahitaji yote muhimu yatakayomsaidia kukua vizuri, kuchunguza zaidi na kuendelea kukua. Mlo kamili utamsaidia kujifunza ladha mpya na kukuza tabia ya kula itakayodumu maishani.

Lakini kumpatia mtoto mlo kamili inaweza kuwa changamoto, hivyo basi usiwe na wasiwasi kama umeshindwa kutimiza.

Vyakula gani mwanangu anahitaji ili kupata mlo kamili?

Vyakula vya wanga

  • Nafaka
  • Tambi
  • Wali
  • Viazi mviringo na viazi vitamu
  • Ndizi za kupikwa
  • Viazi vikuu

Vyakula vinavyotengenezwa na ngano ni vya wanga pia kama mkate. Usimlishe mwanao vyakula vyenye nafaka nzima tu kama unga wa mahindi usiokobolewa, vyakula hivi vinajaza tumbo la mtoto na kupelekea mtoto kuacha kula kabla ya kupata kalori na virutubisho muhumu.

Matunda na mbogamboga

Vyakula hivi ni muhimu kuupa mwili wa mtoto vitamini na madini muhimu yatakayomsaidia mtoto kukua.

Vyakula vyenye madini chuma na protini

  • Nyama
  • Samaki
  • Mayai
  • Karanga
  • Kuku na maharage

Vyakula jamii ya maziwa

Vyakula hivi vina madini ya kalsiamu kwa wingi muhimu katika ukuaji wa mifupa na meno ya mtoto.

  • Maziwa
  • Mtindi
  • Jibini

Maziwa ni chanzo kizuri cha kalsiamu lakini haitaji mengi kama hapo awali alivyokua mchanga. Mpatie 350ml mpaka 500ml kwa siku, usimpatie zaidi ya hapo inaweza kupunguza hamu yake ya kula.

Vyakula gani niweke kikomo kwa mwanangu?

Vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi

Vyakula kama:

  • Keki
  • Biskuti
  • Ice cream

Mwano anahitaji kalori nyingi kumfanya awe na nguvu, lakini vyakula hivi vina manufaa kidogo ya virutubisho. Vinaleta hatari ya mtoto kuwa na kiriba-tumbo.

Vyakula vyenye sukari

Kama pipi na chokoleti, vyakula hivi mwanao asile kila siku. Vina haribu hamu ya mtoto ya kula na kuharibu meno yake.

Vyakula vyenye chumvi.

Watoto wenye mwaka mmoja mpaka mitatu wanatakiwa kg 2 tu za chumvi kwa siku. Miaka 4-6 inaongezeka mpaka 3kg na 7-10 5kg. ni mtihani kuhakikisha mwanao anakula kiwango sahihi cha chumvi kwa siku. Vifuatavyo ni vidokezo vinaweza kukusaidia kumpa mwanaokiwango sahihi:

  • Usiongeze chumvi kwenye chakula chake
  • Weka kikomo kwa mtoto wakokatika ulaji wa vyakula vilivyoandaliwa tayari nje ya nyumbani kama kuku, mishikaki au karanga.

Samaki wenye mafuta

Samaki wenye mafuta ni chanzo kizuri cha omega-3, vitamin na madini. Samaki wenye mafuta kama “mackerel”-samaki wa jamii ya bangala, “salmon”  “fresh tuna” wana mafuta mengi na inashauriwa usimpatie mwanao sana.

Karanga

Ikiwa mwanao ana tatizo la pumu au alegi ya chakula ongea na msahuri wa afya kabla ya kumpatia chakula chenye karanga.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.