Ni vipi unaweza kumsaidia mtoto wako kujifunza kuongea?
Kadri mwanao anavojifunza maneno mapya katika michezo ndivyo anavyoyabeba na kuyatumia kila siku. Zipo njia za kumsaidia mtoto wako kujifunza kuzungumza:
- Zungumza kadri uwezavyo na mwanao. Mtazame usoni na uonyeshe kufurahia anapojaribu kuzungumza na wewe.
- Zingatia zaidi kile ambacho mwanao anajaribu kusema kuliko jinsi anavyotamka matamshi yake. Jitahidi kumfanya mwanao ajisikie huru anapozungumza na wewe.
- Pindi anaposema kitu sahihi, mpatie ripoti sahihi. Kwa mfano, unaweza kumwambia “ndiyo, ni sahihi, hichi ni kijiko”.
- Mfanye mwanao kuona unachomaanisha, kwa kuzingatia unachokifanya na unachozungumza. Unaweza kusema “tunatoa viatu” huku ukimvua viatu vyake kisha “tunaondoa soksi” huku ukimvua soksi zake.
- Pindi unampatia chakula cha mchana mwanao, weka sahani ya chakula mezani kisha mshike mikono na useme “ni muda wa chakula sasa” ataelewa kuwa chakula chake kipo tayari na kitaletwa mezani ikiwa tayari amenusa harufu na kuona maandalizi ya mezani. Anaweza asielewe maana ya “muda wa kula” kama hataona vitendo.
- Chukua usikivu wake kwa kutaja jina lake na kumtazama machoni kabla ya kuzungumza naye. Hii itamsaidia kuelewa kuwa unazungumza naye.
- Mpe mwanao nafasi nyingi za kuzungumza katika kipindi chote cha shughuli za kila siku. Kama unamuuliza swali muache kwa sekunde 10 ili apate muda wa kukujibu.
- Fafanua hali mbalimbali kwa kumtambulisha maneno mengi. Nenda naye matembezi kwenye daladala, mtambulishe vitu anavyoviona na vielezee kwake.
- Rudia kusema kile ambacho mwanao amejaribu kukuambia, hata kama hajatamka kwa ufasaha. Rudia kwa ufasaha kile alichotamka mtoto wako.
- Rahisisha mazungumzo yako. Tumia sentensi fupi na zingatia maneno muhimu unapozungumza na mwanao. Hii itamsaidia kuzingatia taarifa muhimu.
- Zima sauti nyingine zisizohitajika kama vile televisheni na redio. Hii itamsaidia mtoto kukusikiliza kwa umakini unapozungumza naye. Mtoto anapata tabu zaidi kuliko mtu mzima anaposikia kelele.
Nawezaje kumfundisha mtoto kuzungumza kwa kufurahia?
Ni rahisi kupata motisha kwa kufanya kitu unachofurahia. Hivyo utakavyoweza kuzungumza kwa kufurahi na mwanao, hii itamsaidia mtoto kutumia maneno kuweza kujielezea.
Kaa chini sakafu na cheza na mwanao. Muache achague mdoli au mchezo na uzungumze kile anachokifanya. Kwa kujumuika katika michezo na mwanao utampa nafasi nyingi za kumsikia kile anachozungumza kwa mifano sahihi.
Uwe na muda wa kumuigizia mdoli wake anayempenda zaidi kwa vitendo. Mchanganye mdoli wake katika shughuli za kila siku. Mkalishe mdoli wake mezani kwa ajili ya chai na uanze kuzungumza naye kwa kinachofanyika pale.
Angalia vitabu ukiwa na mwanao hata kama hutamsomea hadithi lakini atasikiliza na kujifunza zaidi utakapokuwa unazungumzia picha.
Furahi na mwanao kwa kuimba nyimbo za darasa la awali, kwa kuwa kadri unavyofanya hivyo ndivyo ambavyo mtoto wako atapenda kujiunga.
Cheza na mwanao michezo kwenye simu, hii itamsaidia zaidi kujifunza kuchangia katika mazungumzo.
Jaribu kusikiliza michezo kama vile:
- Michezo ya kupiga makofi, piga kwa mtiririko maalumu kisha subiri kuona kama mtoto wako naye atafanya hivyo.
- Chagua picha sahihi ya sanamu za wanyama na utengeneze sauti kwa mnyama mmojawapo kwa mfano “moo” kisha usubiri mwanao achukue sanamu ya ng’ombe kati ya sanamu ulizomuwekea.