Mazoezi na michezo ifuatayo kwa mwanao yatamsaidia katika ukuaji wa kimwili ni rahisi kujumuisha mazoezi haya katika utaratibu wa kila siku. Utagundua mwanao anakuwa imara na mwenye furaha.
- Kupanda, kukwea kitu
- Kuchora na kuandika haraka bila mpangilio kwenye karatasi
- Kuvaa na kuvua nguo
- Kujaza na kumwaga kwenye makopo yake ya kuchezea
- Kufinyanga/unda na kubomoa
- Kuvuta na kusukuma
- Kuviringisha na kuendesha baiskeli
- Kukimbia na kuruka
- Kuogelea na kuchezea maji
- Kurusha na kudaka