Miezi 20, wiki ya kwanza
Jinsi mtoto anavyokua
Mtoto wako anaweza kukimbia japo hajawa imara vizuri. Anaweza kupanda ngazi mwenyewe, japo atahitaji msaada kutoka kwako kidogo. Anaweza kupenda zaidi kucheza kadiri anavyojifunza jambo jipya kama kurusha vitu.
Watoto wana shahuku ya kila kitu ikiwemo sehemu zake za siri. Mtoto wako anaweza kuanza kuchezea sehemu zake za siri kama alivyokua anachezea mikono na miguu yake akiwa mdogo. Ni jambo la kawaida kabisa, inaweza kuwa jambo lisilo la kawaida kama atachezea sehemu zake za siri mara kwa mara.
Akiwa anachezea sehemu zake za siri mbele za watu mkanye kwa upole na kumuelewesha, sio jambo zuri kufanya hasa mbele za watu.
Ni wakati mzuri wa kuonana au kuwasiliana na mshauri wako wa afya na kumuelezea lolote amablo linakupa wasiwasi kwa mwanao au kwako mwenyewe.
.
Miezi 20, wiki ya pili
Jinsi mtoto anavyokua
Mwanao ataanzisha tabia kama kupiga, kusukuma, kung’ata au kuvuta ili kupata usikivu wako.
Jaribu usiwe mkali katika tabia hizi za mwanao.jaribu kutilia. Tambua anavyojisikia, na muonyeshe wazi kuwa hasira hakikubaliki. Ikiwa mwanao anamuiga ndugu yake mkubwa, jaribu kumuonya kaka au dada yake aonyeshe mfano mzuri kwa mdogo wake.
Wewe ndiye rafiki wa kwanza wa mwanao, utagundua sasa anaanza kujumuika na wenzake. Mtie moyo mwanao kutengeneza marafiki kwa kumpa mfano mzuri. Tabasamu na sema wasalimie marafiki zake anaocheza nao au watoto wengine sehemu za michezo,kwa kufanya hivi mtoto wako ataanza kufuata mwendo wako.
Miezi 20, wiki ya tatu.
Jinsi mtoto anavyokua
Jaribu kufanya mda wa kuoga wa furaha kama mwanao hapendi kuoga. Anzisha mchezo au tabia ya kumchanganya wakati wa kuoga kwa kumuimbia wimbo wa kijinga wenye kufurahisha au mruhusu aoge na mdoli wake anaoupenda.
Miezi 20, wiki ya nne.
Jinsi mtoto anavyokua
Usishangae pale mwanao atakapolia kwasababu luninga imezima ghafla, hii ni dalili ya kuonyesha uelewa wake wa mazingira anayoishi unakua. Kama amezoea jambo fulani likibadilika atakasirika. Kuwa mvumilivu uwezavyo. Hivi karibuni ataweza kukubaliana na mabadiliko haya madogo yanayoweza kumkatisha tama.