Mtoto Mwaka 1 na Miezi 7 – (Miezi 19)

Miezi 19 wiki ya 1

Jinsi mwanao anavyokua

Katika mwezi huu mwanao anaweza kuanza kuelewa wakati vitu haviko sawa au vimemchanganya. Anaweza akaanza kucheka ukichanganya majina ya wanyama, au akashangaa kukiwa na uchafu kwenye sakafu. Hii huonyesha namna mwanao anavyojifunza, na kutengeneza picha namna dunia inavyoenda

Unaweza usielewe kila kitu mwanao anachokisema kwa sasa. Anaweza kuanza kuweka baadhi ya maneno pamoja kama vile mimi taka, mimi enda. nk.

Anaweza kufuatilia kila unachokifanya ili aweze kujua kila kitu unachokifanya kila siku. Mwanao anavyozidi kuwa na uwezo wa kula mwenyewe, anatakiwa aanze kutumia sahani saizi yake na vijiko pia.

Miezi 19 wiki ya 2

Jinsi mwanao anavyokua

Hatakama mwanao ni mchangamfu kwa kipindi kirefu kutakua na nyakati mwanao anaweza kulia na kulalamika sana. Hii inaweza kuwa sababu ya kukujulishwa kuwa ana njaa au amechhoka au anaumwa.

Mwanao wa miezi 19 anajifunza vitu vipya na kuongeza ujuzi kwenye vile anavyochukia, ni jambo la kawaida na anaweza kuonyesha kwa njia ya kulia kulalamika na hata kufanya kiburi.

Mwonyeshe mwanao kwamba unajua amechukia, na unatambua hisia zake. Kama analia na kukung’ang’ania msaidie kusahau hali yake mbaya mkumbatie na mshauri acheze mchezo gani, kama bado analalamika mwambie achague anataka nini.

Kumbukumbu ya mwanao inavyoongezeka, anaweza kutambua ukiumwa unapaswa kwenda hospitali,au anaweza kuogopa akikumbuka alipata chanjo yake katika hospitali.

Kufanya iwe rahisi kwa mwanao beba mdoli ampenda, na baadhi ya vitabu kumfanya awe mchangamfu wakati mnasubiri. Unaweza pia kuuliza kama daktari anaweza kuruhusu akae kwenye mapaja wakati wa uchunguzi.

Miezi 19 wiki ya 3

Jinsi mwanao anavyokua

Ni ngumu kumdanganya mwanao aende kulala, hata baada ya kutulia na kujianda kwenda kulala. Anaweza kutulia lakini mambo yanayomzunguka bado yanamvutia hata akiwa kitandani. Sauti ya luninga au watu kuongea inatosha kumfanya afikiri kwamba kuna kitu kizuri kinaendelea .

Usikasirike kama mwanao amegoma kulala wakati wewe umechoka.

Mwanao anaweza kupunguza muda wa kulala na kutaka maji ya kunywa au kitu cha kula, jaribu kukubali  kubaki katika utaratibu wako wa kila siku, mjuze wakati wa mwisho wa kula au wa kunywa ili usisumbuke.

Kama unampeleka mwanao dukani hakikisha safari ya dukani ni fupi iwezekanavyo ili kukwepa mwanao kutamani vitu, weka midoli ya mwanao ndani ya pochi au begi vitakavyokusaidia kumtuliza mwanao wakati akiwa analalamika na kulia mbele za watu.

Miezi 19 wiki ya 4

Jinsi mwanao anavyokua

Kupanda kwenye vitu ni jambo zuri ila inabidi uwe mwangalifu sana na uhakikishe unakuwa mwangalifu na maeneo ya kupanda kwa watoto. Kuweka vikwazo na vizuizi itasaidia mwanao kushindwa kupanda sehemu hatari.

Kuanguka ni jambo la kawaida na la kutisha, makabati, luninga, ni maeneo ya kawaida ya kutisha kwa mtoto hivyo ni vyema kufanya utaratibu wa kuyakinga maeneo hayo.

Kama mwanao anaamka usiku na kuanza kulia, jaribu kujua kwanini usingizi wake unaingiliwa. Anaweza akawa anaota ndoto mbaya, anapotulia unaweza kumwimbia nyimbo za kumliwaza baada ya hapo unaweza kumrudisha akalala.

 

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.