Miezi 18 wiki ya kwanza
Jinsi mwanao anavyokua
Unaweza kuanza kuona mabadiliko madogo madogo ndani ya mwezi huu, mtoto anaweza kuanza kujiamini sana katika miguu yake na kupenda kupanda juu ya makochi na viti, anaweza pia kuungana na wewe katika kucheza na kukimbia huku na kule.
Baadhi ya siku mwanao anajihusisha katika michezo inayochosha, kama inawezekana mpe muda wa kuwa nje kila siku na kama hali ya hewa sio nzuri sana mpatie lisaa limoja au mawili ya kucheza katika chumba chenye michezo mingi.
Mwanao hatahitaji viatu mpaka atakavyoanza kutembea nje.
Miguu ya mtoto mchanga inaweza kuumia kirahisi kwahiyo tembelea duka la viatu au sokoni kwa ajili ya kupata kiatu kitakachomfaa mwanao vyema.
Miezi 18 wiki ya 2
Jinsi mwanao anavyokua
Utagundua mwanao hapendi kulala, lakini anapendelea kutembe na kukimbia.Kumbuka kubeba kiti cha mtoto ili usiumie mgongo kama unaenda safari ya mbali.
Mwanao anavyozidi kusema sitaki kila mara unaweza kuwaza namna gani utaweza kummudu. Mkumbushe kila mara jambo lipi ni zuri kufanya na lipi sio sawa kufanya itamsaidia kuelewa zaidi.
Kuwa mfano wa kuigwa,muonyeshe tabia njema,utu hii itamsaidia mwanao kuchagua kitu bora cha kufanya au njia nzuri ya maisha
Miezi 18 wiki ya 3
Jinsi mwanao anavyokua
Hakuna umri husika wa kumwamishia mwanao katika kitanda kikubwa, mwanzishie mwanao kulala kwenye kitanda kikubwa ili mtoto mwingine anapokuja asijisikie kama amenyang’anywa kitanda chake.
Kama mwanao anapenda kitanda chake na hana shida hamna haja ya kumwamisha, tambua tu kwamba mara mwanao anapokua kitandani, anaweza kuamka wakati wowote usiku.
Kwa sababu hiyo wazazi wengi wanashauri umwache mwanao katika kitanda chake muda mrefu uwezavyo.
Baadhi ya watoto hawashuki kitandani hatakama ni wakubwa kiasi gani, wengine hushuka mapema waezavyo kama inawezekana chukua hatua mapema kuweza kumdhibiti mwanao ili kuepusha madhara.
Miezi 18 wiki ya 4
Jinsi mwanao anavyokua.
Uwezo wa mwanao wa kuongea utaongezeka, maneno yake ya kwanza yanaweza kuwa mama, baba, dada, maneno mengine hufuata baadaye zaidi katika miezi inayofuata.
Katika watoto wanaoongea kuna wengine hawataongea sana, usiwe na wasiwasi kama mwanao hajaongea bado, lakini kama hajaongea hata neno moja mpeleke kwa daktari wako ili aweze kukusaidia upate kumwona mtaalamu wa kuongea kwa watoto
Katika kipindi hiki ni vyema ukatumia mafuta ya kumlinda mwanao kwenye jua ili asipate madhara ya kuungua na jua na kuweza kupata kansa ya ngozi hapo baadae, kwahiyo mlinde mwanao mtokapo nje kila mara, hatakama hali ya hewa inaruhusu mpake mafuta ya kumlinda.