Miezi 17 wiki ya 1
Jinsi mwanao anavyokua.
Ikiwemo kunyooshea vitu kidole vile vinavyomvutia, mwanao sasa anaweza akawa anasema maneno tofauti tofauti, anaweza akawa anavua nguo mwenyewe na sio kuvaa, kuchana nywele na kula pia.
Anaweza kutaka kusafisha kinywa chake mwenyewe na kupiga mswaki ingawa bado anahitaji msaada wako juu ya hilo.
Kama mwanao sio mlaji sana, fanya ulaji uwe kidogo kidogo ila mara kwa mara mpe achague anataka kula nini kila wakati.
Anachokula ndani ya wiki ni bora kuliko anachokula katika mlo mmoja.
Miezi 17 wiki ya 2
Jinsi mwanao anavyokua
Je mwanao ameanza kupiga kelele kila mara anapotaka umsikilize? Anajifunza, na wewe utatambua kuwa sauti yake inaweza kufanya mengi zaidi ya kukufanya umsikilize.
Ni vyema ukamweleza kua kupiga kelele sio vizuri na inakuumiza masikio na inaweza kukufanya ushindwe kumsikia pale atakapokuwa akikuita hivyo atapunguza na kuacha kabisa kupiga kelele kila mara.
Kuvimbiwa ni kawaida kwa watoto,hivyo ulaji mwingi wa vyakula ambavyo ni vyanzo vya nyuzinyuzi (fiber) na maji au vimiminika vya kutosha itamsaidia sana.jaribu kumpa vyakula ambavyo ni vyanzo vya nyuzinyuzi (fibe)r kama maharage mahindi matamu nk.
Miezi 17 wiki ya 3
Jinsi mwanao anavyokua
Je mwanao anashindwa kwenda popote bila mdoli wake?
Hiki ni kitu cha kawaida kabisa kwa umri wake, mwanao anakua kimwili na kiakili na kila siku hukaririwa kwa ishara, sauiti au maneno fulani.
Kumkumbatia mdoli humfanya awe na furaha na kujihisi yuko salama, haswa kama haupo au anaumwa au amechoka.
Kuwa na kitu cha kumlinda ni ishara ya ukuaji, mwanao ameanza kuwa na hisia ya tofauti, ili kuepuka kulia kuwa na mdoli wa ziada wa kufanana.
Kama mwanao anavyozidi kujiamini kwa kusimama na kutembea mwenyewe, itabidi ufanye jitihada za kila hali kumfanya awe salama. Ajali za mara kwa mara kama kuanguka kwenye ngazi, kiti au meza na kuungua pia ni jambo la kawaida.
Kulamba sumu za vifaa vya usafi au dawa pia ni jambo la kawaida,
Miezi 17 wiki ya 4
Jinsi mwanao anavyokua
Mtoto anaweza kufanya kioja wakati analia na hali hii inaweza kukutia hasira sana hasa kama amekatazwa kufanya jambo fulani au haruhusiwi au akiwa na njaa.
Itakupasa kumbembeleza mwanao na kumwondolea hasira alionayo kwa ajili yenu wote. Utatambua kuwa kulia kwa mwanao kutaisha mapema bila wewe kutaka kujua analia kwa sababu gani nini kwa dakika kadhaa. Alafu ndipo umbembeleze kwa maneno mazuri.
Atakapotulia mkumbatie,usimwadhibu. Katika umri wake hawezi kujizuia bali kuwa na hasira mara kwa mara. Lakini jitahidi kumridhisha anachotaka ili kuepuka kulia kwake, lakini sio kila jambo ni lazima umpatie, jaribu kumridhisha kwa mambo ya muhimu tu.