Mtoto Mwaka 1 na Miezi 4 – (Miezi 16)

Miezi 16 wiki ya kwanza

Jinsi mwanao anavyokua

Mwanao anajifunza zaidi kuhusu ulimwengu kila siku. Ambapo miezi michache iliopita alikuwa akiweka kila kitu mdomoni na sasa anaweza kutambua matumizi ya kila kimoja pekee yake.

Anaanza kucheza michezo mbalimbali na anapendelea zaidi mchezo wa kuona, au kutaja sehemu za mwili, kumbukumbu yake nayo inakua na hata hivyo anaweza kukumbuka mambo mbalimbali ambayo unaweza ukawa umeyasahau.

Ingawa mwanao anaweza akawa anacheza kila mahala na kuhangaika anaweza asiwe mkakamavu miguuuni anaweza kusahau hatua mbalimbali za ngazi, au akajikwaaa kwenye miguu yake akiwa anakukimbilia umkumbatie, ni vyemba ukawa na boksi la huduma ya kwanza ndani ya nyumba yako.

Miezi 16 wiki ya 2

Jinsi mwanao anavyokua

Unaweza ukawa unawaza ni lini inafaa zaidi kuanza kumwadhibu mwanao haswa pale afanya kosa, inaweza ikawa hafanyi makusudi ila anaangalia kipi anaweza kufanya na kipi hawezi kufanya akiwa na wewe

Wakati mwingine anaweza akawa mdadisi tu.

Ni sawa kujua kuwa anajifunza ila haimaanishi atakuwa na tabia nzuri hapo mbeleni ukimwacha.

Namna uwezo wa mwanao wa kuongea unavyozidi, endelea kumsomea hadithi kumwimbia na kuongea nae kila mara ili kuongeza uwezo wake zaidi.

Miezi 16 wiki ya 3

Jinsi mwanao anavyokua.

Kati ya sasa na miezi 18 utaanza kutambua mwanao ameacha kulala asubuhi lakini bado anahitaji kulala mchana hakikisha isiwe jioni ili aweze kulala ifikapo usiku.

Mwanao bado anaweza akawa anahitaji kupumzika ifikapo asubuhi, sio lazima alale bali anaweza kupumzika tu kuangalia katuni kukaa kwenye kochii na kusikiliza mziki laini.

Mwanao anapenda kuangalia luninga wataaalamu wanashauri dakika 10 au pungufu ni bora zaidi kwa mtoto, tambua kwamba mtoto chini ya miaka 2 haishauriwi na wataalamu kuangalia luninga.

Miezi 16 wiki ya 4

Jinsi mtoto anavyokua.

Watoto wanaweza wakawa wanachekesha hata kama wanafanya kitu ambacho hawajaruhusiwa, kama vile kupanda juu ya meza kutumbukiza vitu chooni nk.

Mwanao anaelewa vingi kuliko unavyodhani, ikiwemo ishara za mwili. Ukimwambia aache wakati unacheka ataona ni mchezo na ataendelea ila ukiwa hucheki na ukimwabia aache ataacha mara moja na kujua unamaanisha.

Jaribu kuwa msisitizaji uwezavyo, ukimkataza kitu sasa na kuacha kumkataza baadae utamchanganya mtoto na kushindwa kuelewa afanyeje .

Utakuta mwanao wa miezi 16 anaanza kukataa kufungwa mkanda wa gari, akikataa mweleze sababu ya kufunga mkanda na mkubaliane ili afunge mkanda. Na mwendelee na safari.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.