Wiki ya kwanza ya miezi 13
Jinsi mtoto wako anavyokua
Je,mtoto wako ameanza kutembea hata hatua moja,kama bado atapiga hatua mda sio mrefu, ni vyema kuweka kamera yako karibu ili kupata picha nzuri, baadhi ya watoto hawatembei mpaka miezi 16 au 17 wengine hata baadae.
Kama mtoto wako hajaanza kutembea atazidi kutamani kujua vinavyomzunguka. Usishangae akaanza kuupaka ukuta chakula haswa sasa kipindi ambacho ameanza kuwa na kutumia mikono yake.
Ukitaka kusafiri inabidi ujiandae kwa sasa inakuwa ngumu sana. Hatakama unaenda tu kuendesha gari au unapanda ndege kwa safari ndefu.
Paki vyakula rahisi kula, na usisahau maji na maziwa, pia nepi na taulo zenye unyevuunyevu. Beba koti au sweta kwa ajili ya mtoto kama hali ya hewa itabadilika. Na nguo nyingine za ziada zako na za mtoto wako huwezi kujua ni wakati gani unaweza ukachafuka.
Mdoli unaopendwa na mtoto wako anaweza kumsaidia mtoto wako ajisikie yuko mbali na nyumbani wakati anasafiri haswa safari ndefu.
Miezi 13 wiki ya 2
Jinsi mtoto wako anavyokua
Kwa mtoto wa miezi 13, ulimwengu unaomzunguka ni sehemu kubwa ya kufanya ni utafiti mkubwa anaopendelea kufanya
Sio kwamba ni msumbufu bali anafuraha ya kujaribu kila anachokiona na kwamba anaweza kufanya baadhi ya mambo, hivyo unaweza kumwona akiangusha vitu huku na kule kila mara.
Michezo ya watoto ya kuweka na kutoa vitu kwenye kontena inaweza ikawa yakufaa zaidi
Miezi 13 wiki ya 3
Jinsi mtoto wako anavyokua
Mwanao anaanza kujua sauti mbalimbali, na anaweza kuanza kuonyesha hisia zake kwa ishara na kulia kwa sauti, na anaweza kuanza kufurahi kuwa na wenzake.
Mchezo wa kujificha- mtoto kujificha usimwone na kungoja umkamate kwa furaha, unaweza kuwa moja kati ya michezo ya mtoto wa miezi 13. Kama kujificha nyuma ya kiti, chini ya meza au kwenye pazia humfurahisha sana mtoto.
Mchezo wa kutafuta: kurusha vitu kutoka kitandani kwake na kukiokota tena, au kuangusha kijiko na kumpatia adondoshe na yeye kunampa mtoto furaha sana na kumfanya augeuze kuwa mchezo wa furaha
Niangalie mama: mwanao anapenda kuangaliwa na kuwa na shabiki, na kurudia chochote utakacho kifurahia. Kuwa makini kufurahia kitu chanya na kukataza kile kibaya mara moja
Maigizo: kaa pembeni ya mwanao na ufanye kitu kidogo na cha kufurahisha ili mwanao aigize kama wewe, kama vile kupiga makofi, kuziba uso nk. Msifie mwanao kama ataweza kukuiga vyema.