Je, umri wangu unaathiri uwezo wangu wa kuzaa?
Ndio. Uwezo wa kuzaa unaanza kupungua kwa wanawake kuanzia umri wa miaka 30, na kushuka kwa kasi zaidi kuanzia miaka 35. Kadiri umri unavyoendelea kwa wanawake uwezekano wa kupata mimba unapungua, na uwezekano wa kuwa tasa unaongezeka.
Wanawake wengi wataweza kuzaa kwa njia ya kawaida na kujifungua watoto wenye afya kama watapata mimba wakiwa na umri wa miaka 35. Baada ya miaka 35, kiasi cha wanawake wenye matatizo ya utasa,kuharibika mimba au matatizo ya watoto wanaozaliwa yataongezeka. Katika umri wa miaka 40 ni wanawake wawili tu kati ya watano wanataka mtoto, watafanikiwa kupata mtoto.
Wanaume wanaweza kuwa na uwezo wa kuzaa kwa mda mrefu zaidi kuliko wanawake .Ingawa uzazi wa mwanaume pia unapungua kwa umri,na kutokea hatua kwa hatua kwa wanaume.
Wakati wanaume wengi wanabaki na uwezo wa kuzaa katika miaka 50 na zaidi, idadi ya wanaume wenye ugonjwa wa manii huongezeka kadiri umri unavyoongezeka. Kupungua kwa uwezo wa kuzaa kwa wanaume ni wa hatua kwa hatua kuliko wanawake. Kupungua kwa uwezo wa kuzaa kwa wanaume kunaathiri afya ya watoto ambao watazaliwa.
Kiukweli, kadiri unavyokua mkubwa, ndivyo unavyokua katika hali ya kujifungua mapacha wasiofanana. Inafikirika kuwa mwili wako unatarajia kutoa zaidi homoni zenye kusaidia mayai yapevuke kadiri umri unavyoongezeka. Homoni inajulikana kama Follicle Stimulating Hormone (FSH) hutengenezwa zaidi kwasababu mayai yanayofaa yamebaki machache katika ovari zako.
Utengenezaji zaidi wa FSH unapelekea upevushwaji wa mayai toka kwenye ovari kwa wingi. Matokeo? Yai zaidi ya moja linarutubishwa na mtoto zaidi ya mmoja hutokea.
Unaweza kufurahishwa kujua unategemea kuwa na mapacha. Kwa baadhi ya wanawake kuwa na mapacha inatimiza ndoto yao ya kuwa na watoto zaidi ya mmoja katika ujauzito mmoja. Ila pia ni muhimu kuweka akilini kwamba kuwahudumia mapacha inahitaji zaidi muda wako,hisia na uchumi zaidi ya kuhudumia mtoto mmoja.
Je, itachukua muda mrefu kuzaa kadiri ninavyokua mtu mzima sana?
Uwezo wako wa kuzaa haraka unategemeana na umri wako. Wanawake wanakua na uwezo wa kuzaa miaka ya 20 na 24. Itachukua muda sana kupata mimba ukifika miaka ya 30 mwishoni au miaka ya 40 mwanzoni.
Zaidi ya asilimia 80 ya wanandoa watazaa ndani yam waka wa kwanza kama wataacha kutumia njia za uzazi wa mpango na kujamiana mara kwa mara. Kujamiana mara kwa mara inamaanisha kufanya mapenzi mara mbili au tatu za mzunguko wote. Hii inakupa nafasi nzuri ya kupata mimba.
Karibu nusu ya wanawake ambao hawana mimba katika mwaka wa kwanza watapata mimba mwaka unaofuata, kutoa kiwango cha ujauzito wa asilimia 92 ndani ya miaka miwili. Kwa hivyo hulipa kuendelea kujaribu.
Kwa sababu viwango vya njia za uzazi wa mpango ni vizuri kulingana na mda, mara nyingi inapendekezwa kupata msaada kutoka kwa mtaalamu wako wa afya ikiwa hujafanikiwa kupata mimba baada ya mwaka wa kufanya ngono ya kawaida (mara mbili hadi tatu kwa wiki)
Kwanini uwezo wa kuzaa unapungua kwa haraka zaidi?
Vyanzo vikuu viwili vya utasa kwa wanawake ni matatizo yatokanayo na kupevuka kwa yai na kuziba kwa mirija ya falopiani kama matokeo ya maambukizi.
Matatizo yatokanayo na upevushwaji wa yai yanatokea kadiri unavyozidi kuongezeka umri kwasababu:
- Una mayai machache mazuri yaliyobakia, hivyo inafanya ugumu kushika mimba. Idadi ya mayai kwenye ovari hupungua kadiri ya umri
- Wanawake wachache (asilimia moja) wanapitia kukoma kwa hedhi (menopause) mapema zaidi kuliko kawaida, na mayai kuachwa kupevushwa kabla ya kufika miaka 40.
- Hedhi inakua tofauti (isiyo kawaida). Unapokaribia kipindi cha kukoma kwa hedhi, hedhi yako inakua pungufu na upevushwaji wa mayai kuendelea kupungua au kuwa tofauti na kawaida.
Kuziba kwa mirija ya falopiani kunaweza kusababishwa na maambukizi au tatizo linguine. Hivyo, haijalishi umri wako, ila unapotafuta motto inabidi kuwa mwangalifu. Hii inamaanisha kuwa mwangalifu na maisha yako ya kimapenzi na vile vile afya kwa ujumla.
Mwanamke anapoongezeka umri, yuko katika hali ya kuwa na magonjwa ambayo hayajatibiwa muda mrefu. Mfano klamidia isiyotibiwa kwa mda mrefu inaweza kukua na kusababisha maambukizi ya mfumo wa uzazi wa mwanamke (PID), kuziba kwa mirija ya falopiani. Hii inaweza kuzuia urutubishwaji wa yai la mwanamke au kuongeza uwepo wa mimba nje ya mirija ya uzazi.
Hali zinazoweza kuathiri uzazi ni pamoja na:
- Endometriosis ni ugonjwa ambao huhusisha seli zinazofaa kuwa ndani ya mji wa uzazi kuwa nje ya mji huo. Ikiwa una ugonjwa huu, madhara yake huongezeka kadiri unavyokongezeka umri. Uharibifu katika mirija yako ya falopiani unaweza kusababisha mimba nje ya mirija ya uzazi.
- Fibroids ni uvimbe katika kizazi jina linguine myomas, ni matatizo ya kawaida kwa wanawake miaka 30 na zaidi na huweza kusababisha matatizo ya uzazi.
Kumbuka kuwa na uzito mkubwa kunaleta ugumu wa kupata mimba. Kupungua uzito kunaweza kukusaidia kushika mimba kama una tatizo la ugonjwa wa “chango” kwa wanawake (PCOS).