Je, ni lazima kuwa na uzito wenye afya kabla ya kujaribu kupata mtoto?
Ni wazo zuri. Kuwa na uzito wenye afya kutaimarisha nafasi ya kushika mimba na kuzaa. Uzito mzuri kiafya ni kati ya BMI 19 na 25.
Kama una uzito kubwa, kupungua uzito kutapunguza hatari ya luwa na magonjwa ya kiafya kwako na mtoto, hasa kama uzito wako ni BMI 30 au zaidi. Inaweza kuboresha uzazi wako pia.
Kufuata mlo bora na kujiweka imara sasa kutakupatia mwanzo mzuri wa ujauzito.
Kama una uzito pungufu,zungumza na mshauri wako wa afya kuhusu njia nyingine za kiafya za kuongeza uzito wako. Una uwezekano zaidi wa kuwa na mzunguko wa hedhi usio wa kawaida, ikiwa una uzito pungufu. Hali hii inafanya ugumu wa kushika mimba, hasa kama unakosa siku zako.
Kwa bahati nzuri, kwa kesi nyingi, kufanikiwa kupata uzito wenye afya kutarudisha mzunguko wako katika mstari.
Je, niache kuvuta sigara, kunywa na kutumia madawa ya kulevya kabla ya kujaribu kupata mtoto?Ndio. Kuvuta sigara na kunywa pombe zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya afya kwa mtoto kama una mimba. Zinaongeza pia hatari ya kuharibika kwa mimba. Na hakuna dawa hata moja isiyoshauriwa na daktari ambayo ni salama kwa wanawake wajawazito na watoto wao.
Ukiwa mjamzito ni vema kujua mapema. Hivyo basi, ni vema kuacha bidhaa hizi hatarishi sasa, na kumlinda mtoto wako katika siku hizi muhimu za kwanza.
Kuacha kuvuta sigara kunaweza kuwa ngumu, lakini unaweza jaribu mpaka mara tano na kufanikiwa na kwa usaidizi wa mshauri wako wa afya.
kwa upande wa pombe, kitu salama ni kuacha kabisa. Hakuna njia ya kujua ni kiasi gani cha pombe ni salama kipindi cha ujauzito. Ingawa, inajulikana kwamba unavyozidi kunywa, ndivyo hatari za kiafya kwa mtoto wako zinaongezeka. Pia, pale unapohitaji msaada kuacha pombe, ongea na mshauri wako wa afya, atafurahi kukushauri. Na pia kama unatumia dawa za kulevya ni bora kumshirikisha mshauri wako wa afya ili akusaidie.
Je, nimuone mshauri wangu wa afya kabla sijajaribu kupata mtoto?
Ni muhimu kumuona mshauri wako wa afya kama una matibabu ya mda mrefu ya asthma, kisukari au kifafa.
Kama unatumia dawa, unaweza hitaji kufanya mabadiliko ya matibabu yako. Hii ni kwasababu baadhi ya aina za dawa sio salama kutumia ukiwa mjamzito, na inaweza chukua wiki kadhaa kabla ya kujua una mimba. Lakini hata hivyo, haishauriwi kuacha kutumia matibabu bila kujadiliana na daktari wako kwanza.
Kama itakubidi kubadilisha matibabu, mwili wako utahitaji mda ili kuendana na marekebisho yaliochukua nafasi. Hivyo ni vizuri kuonana na daktari wako angalau miezi mitatu kabla ya kujaribu kupata mtoto.
Je, nitarajie nini katika vipimo vya awali kabla ya kujaribu kupata mtoto?
Kama ukiamua kufanya vipimo vya awali kabla ya kupata mimba, mtaalamu wako wa afya au nesi anaweza kukuliza kuhusu:
- Kama kazi yako inahusisha kufanya kazi na vitu hatari
- Kama una matatizo na siku zako za hedhi
- Hali yako ya afya na maisha kiujumla
- Mazoezi kiasi unafanya
- Hali yako ya kihisia(emotional wellbeing)
- Tabia yako ya kula
Daktari wako atapenda kujua hali yoyote ya kiafya ulionayo, kama:
- Kisukari
- Asthma
- Shinikizo la damu
- Kifafa
- Matizo ya tezi
- Matatizo ya moyo
- Magonjwa ya akili
Mambo mengine yakujadili katika vipimo hivi vya awali kabla ya kushika mimba ni kama:
- Hali ya magonjwa ya kurithi katika familia yenu. Mueleze mshauri wako wa afya kama kuna historia ya magonjwa ya kurithi katika familia yenu kama siko seli, magonjwa ya mfumo wa upumuaji(uvimbe wa viriba hewa) au anemia
- Uzazi wako wa mpango. Mara nyingi, njia za uzazi wa mpango ulizotumia haziwezi kuathiri mda gani umekaa kupata mimba. Lakini kama ulikua unatumia sindano, inaweza kuchukua mpaka mwaka mmoja baada ya sindano yako ya mwisho, taratibu za uzazi wako kurudi hali ya awali.
Daktari wako anaweza kuuliza kuhusu mimba ulizotoa, zilizoharibika au kutungwa nje ya uterasi(ectopic pregnancy), ingawa kuongelea matukio haya kunaleta huzuni ni vizuri kumwambia daktari wako ili kupata ushauri na huduma nzuri sasa.
Je, nifanye vipimo vya matibabu kabla ya kujaribu kupata mtoto?
Unahitaji kufanya, ila inategemea na hali yako na afya kwa ujumla. Muulize mshauri wako wa afya au muuguzi kama inahitaji kufanya vipimo kabla ya kushika mimba. Uchunguzi wa kawaida na vipimo kabla ya ujauzito ni pamoja na: Vipimo vya magonjwa ya zinaaKama uliwahi kufanya ngono isio salama, ni vema kufanya uchunguzi wa magonjwa ya kuambukizwa ya ngono, hatakama hakuna dalili. Ni vema kufanyiwa vipimo vya:· Homa ya ini· Klamidia· Kaswende· Virusi vya Ukimwi(HIV) Kufanya matibabu ya magonjwa ya ngono mapema kabla ya kupata mimba kunaongeza nafasi ya kuwa na mafanikio kwenye ujauzito.
Vipimo vya kizaziIkiwa unatoka kufanya uchunguzi wa kizazi ndani ya mwaka ujao, unaweza kufanya kabla ya mimba. Hii ni kwa sababu uchunguzi wa kizazi haufanyiki wakati wa ujauzito, kwani mabadiliko ya asili ya kizazi chako hufanya matokeo kuwa magumu kufsiri.
Vipimo vya damuIkiwa unafanya vipimo vya awali kabla ya mimba, na mshauri wako wa afya au muuguzi wako akawa na wasiwasi una anemia, atakushauri ufanye vipimo hivi. Hii ni kwasababu wanawake wenye anemia maranyingi wanahitaji kuchukua madini ya chuma ya ziada kipindi cha mimba. Kulingana na asili ya kabila na historia yako ya matibabu, kuna uhitaji wa kufanya vipimo vya magonjwa ya kurithi kama siko seli na anemia. Vipimo hivi vitakupatia uhakika na ufahamu wa kujua ni kiasi gani utamrithisha mwanao hali hizi za kiafya. Ikiwa hauna uhakika kama umepatiwa chanjo ya rubella, unaweza kufanyiwa vipimo vya damu kuangalia.
Je, nipate chanjo kabla ya kujaribu kupata mtoto?
Maambukizi mengi yakuzuilika yanaweza sababisha uharibifu wa mimba au kasoro baada ya kuzaliwa, hakikisha unapata chanjo kwa mda.
Kama unahitaji chanjo ya magonjwa ya virusi kama rubella, inabidi kusubiri mwezi mmoja kabla ya kujaribu kupata mtoto. Hii ni tahadhari, kwani inasadikika mwili wako kuhitaji muda wa kuangamiza kirusi kabla ya kubeba mimba.
Kama uko katika hatari za ugonjwa wa homa ya ini, unaweza kuamua kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huu. Hivyo basi kama hi indo chanjo pekee ulionayo, unaweza kuanza kujaribu kupata mtoto mara moja.